Penguin (Biskuti)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Penguin(Biskuti))
Jump to navigation Jump to search
Pakiti ya Penguin

Biskuti ya Penguin ni aina za biskuti zilizopakwa chokoleti ndani na nje. Zinatayarishwa na sehemu ya kampuni ya United Biscuits ya McVitie's. Biskuti za Tim Tam zilizotayarishwa na Arnott's,Australia ilipikwa kwa njia moja na zile za Australia na ikazua mjadala mkali kuhusu biskuti gani ndizo bora zaidi kati ya hizo mbili.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Biskuti hizi zilitayarishwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1932 na William McDonald, mtayarishaji wa biskuti mjini Glasgow na ikawa bidhaa za McVitie's McDonald alipoungana na McVitie's na Price, MacFarlane Lang & Co na Crawford ili kuunda kampuni ya United Biscuits.

Kila pakiti imeandikwa kichekesho ama ukweli unaochekesha pamoja na michoro ya ngwini inayofurahisha ama picha maarufu za kitambo.

Biskuti za Penguin zilikuwa katika kesi kati ya United Biscuits na Asda waliposhtaki Asda kwa kujaribu kuuza biskuti zao za "Puffin" ni kama ni bidhaa za Penguin. Mahakama ilipata kuwa Asda walikuwa na kosa la kujaribu kufananisha bidhaa zao na za Penguin lakini wakagundua kuwa Asda hawakuwa wamevunja sheria zozote zinazohusu jina la Penguin. United Biscuits imekosolewa sana kwa kuendelea kutumia asidi ya ufuta katika siagi wanayopaka kwa Penguin,ambayo si nzuri.

Hapo mwaka wa 2007,United Biscuits ziliaanza kutangaza kukosekana kwa asidi hiyo ya ufuta katika biskuti za Penguin, baada ya kuondolewa kwa kutayarisha biskuti hizo.

Penguin wako na tangazo maarufu la "P-p-p-pick up a Penguin"(yaani chukua Penguin ) imetumika sana katika vyombo vya habari.

Tangazo lao la P-p-p-pick up a Penguin likionekana kwa pakiti hii

Bidhaa Zingine Mbalimbali[hariri | hariri chanzo]

Aina za biskuti ya Penguin

Katika mwaka wa 2003,McVitie's imeunda bidhaa ndogondogo mbalimbali za aina ya biskuti za Penguin:Penguin Chukkas, Wing Dings,Flipper Dipper, Splatz na Mini Splatz. Bidhaa hizi tofauti zilifuatwa na kampeni ya gharamu ya kufikia £ 5 million. Mnamo mwaka wa 2008,McVitie's ,pia, ilianza kutayarisha biskuti za Penguin Triple Chocolate Wafers. [12]

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

1. ^ Kirsty Needham (2003-04-18). "Branding rivals will never take the biscuit, says Mr Tim Tam". http://www.smh.com.au/articles/2003/04/17/1050172707606.html.10 Oktoba 2006.

2. ^ "Tim Tam dhidi ya Penguin". 2003-01-12. http://www.nicecupofteaandasitdown.com/biscuits/previous.php3?item=48.11 Oktoba 2006.

3. ^ Mike Adamson (2005-08-26). Guardian Unlimited. http://sport.guardian.co.uk/ashes2005/story/0,,1557204,00.html.11 Oktoba 2006.

4. ^ Karen Fong (1997-05-01). "Penguin dhidi ya Puffin". Rouse & Co. International. http://www.iprights.com/publications/articles/article.asp?articleID=60.5 Oktoba 2006.

5. ^ "United biscuits". tfX: http://www.tfx.org.uk/page35.html. Retrieved 5 Oktoba 2006.

6. ^ " Tovuti rasmi ya United Biscuits". http://www.unitedbiscuits.com/80256C1A0047922E/vWeb/pcTSTT5EPGG9.14 Februari 2008.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

  • Picnics past - Observer hadithi kuwa Penguin ndizo biskuti bora kabisa katika miaka ya 1970s