Nenda kwa yaliyomo

Passat (meli)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Passat(meli)

Passat (meli)

[hariri | hariri chanzo]

Passat ni meli ya Kijerumani ya aina ya milingoti minne kwenye ngamani yake na ni mojawapo wa meli za Flying P-Liners, meli maarufu za kampuni ya Kijerumani ya F. Laeisz. Jina "Passat" linamaanisha upepo wa biashara katika Kijerumani. Yeye ndiye mmoja wa meli chache zilizobaki za aina ya WindJammers zinazokazia upepo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ilizinduliwa katika mwaka wa 1911 kwa kiwanja cha Blohm & Voss, Hamburg, meli hii ilitumika kwa miongo mingi kama meli ya shehena mpaka wakati kulikokuwa na meli zilizotumia mvuke. Katika mwaka wa 1932, iliuzwa kwa Gustaf Erikson wa Finland. Meli hii ilishiriki katika "Mashindano ya Meli Za Kitambo" iliyohusu kushindana karibu na Cape Horn na meli zingine za kitambo. Miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa meli hiyo ni Niels Jannasch aliyefanikiwa na kuwa mkurugenzi wa Jumba la Kumbukumbu la Usafiri kwa Atlantiki, Canada. Katika mwaka wa 1951, Passat na Pamir(meli isiyofanana na Passat) zilifanywa meli saidizi katika shule ya meli za umarina zakibiashara za Kijerumani. Miaka sita baadaye,1957,Passat iliachishwa kufanya kazi shule hiyo ya umarina baada ya Pamir kuzama katika dhoruba kali. Passat, pia, karibu izame na kuwa na hatima moja na Pamir wakati shehena yake ilifunguka na kusongasonga.

Meli yenyewe sasa ni nyumba ya kupanga ya vijana, ukumbi, meli ya makumbusho na kumbusho la kihistoria ikiwa imehifadhiwa shamba la Lübeck, Ujerumani.

Dada meli ya Passat

[hariri | hariri chanzo]

Dada meli kwake Passat ni Peking iliyonusurishwa na kuhifadhiwa kama meli ya makumbusho. Peking ni kivutio katika jumba la kumbukumbu la South Street Seaport,bandari ya New York(Marekani). Pamir imejadiliwa mara nyingi kama dada meli ya Passat kwa kuwa meli hizo zilionyeshwa zikiwa pamoja katika picha nyingi za miaka ya 1950. Meli nane za aina ya milingoti minne kenye ngamani zilizonunuliwa na Laeisz zimetajwa kimakosa kuwa "Dada Wanane",kwa kufanana kwao, ni Pangani,Petschili,Pamir,Passat,Peking,Priwall,Pola(meli hii haijawahi kuwa katika kampuni ya Laeisz) na Padua(ambayo sasa inaelea baharini na bendera ya Urusi kama meli ya mafunzo,Kruzenshtern). Kwa meli hizi nane Pangani, Petschili, Pamir na Padua hazikuwa na dada meli za kweli.


Filamu za Passat katika Tovuti

[hariri | hariri chanzo]

Filamu za kweli na za kwanza za 1957 zipo katika filamu ya mafunzo ya Heinrich Klemme,Die Pamir("Pamir",1959)

Kipande kidogo cha filamu hiyo ya Kijerumani inapatikana katika tovuti ya Schiele-Schoen Archived 24 Juni 2013 at the Wayback Machine.,ikionyesha Passat katika sekunde 29 za mwisho ikiwa imenusurika baada ya dhoruba katika mwaka wa 1957.

Angalia Pia

   * P-Liner
   * Pamir (meli)

Viungo vya nje Tovuti Kamili ya Passat(meli) Lübeck Meli ya Makumbusho ya Kijerumani Majina ya Meli Meli Ndefu za Kijerumani Meli za 1911