Pasargadi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tomb of Cyrus the Great,Pasargadae

Pasargadi (pia: Pasargadae, fa. پاسارگاد pasargad) ni mahali pa kihistoria katika jimbo la Fars nchini Uajemi (Iran). Hapa ilikuwepo mji mkuu wa Koreshi Mkuu aliyeanza kuijenga mnamno mwaka 546 KK baada ya kuunganisha Umedi na Uajemi. Wakati ule Koreshi alijiita "Mfalme wa Wamedi na Waajemi" alitaka kuwa na mji mkuu katika kila kati ya sehemu mbili za ufalme wake akitumia Ekbatana kama mji mkuu katika Umedi wakati wa joto na alianzisha Pasargadi kama mji wake katika sehemu ya uajemi kwa ajili ya majira ya baridi.

Hadi kifo cha Koreshi ujenzi wa mji haukukamilishwa bado; wafuasi waliendelea lakini mfalme Dario I alianzisha mji mkuu mpya katika Persepolis.

Kati ya maghofu kuna kaburi 1 iliyotunzwa vizuri na kuaminiwa ni kaburi la Koreshi Mkuu.

Picha za Pasargadi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: