Ombwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Ombwe (ing. vacuum) kwa maana ya sayansi ni hali pasipo na kitu, nafasi pasipo na mata. Neno hutumiwa hasa kwa hali pasipo na gesi au angahewa. Katika lugha nyingi za dunia neno la kilatini "vacuum" hutumiwa.

Hali halisi si rahisi kupata mahali duniani pasipo na kitu chochote kabisa. Mara nyingi anga-nje la ardhi yetu huitwa "ombwe". Lakini hata katika ombwe hii kuna mata kidogo. Kwa hiyo "Ombwe" mara nyingi ni hali ambako kiasi cha gesi au hewa kimepungukiwa sana ndani ya chombo na hapa kuna matumizi ya kiuchumi kwa mfano kutunza vyakula ndani ya mifuko ambako hewa nyingi imetolewa nje na hivyo vyakula vinadumu muda mrefu zaidi kwa sababu ya uhaba wa oksijeni ndani ya mfuko.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]