Omar Khayyam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Picha ya Omar Khayyam

Omar Chayyām (Kifarsi: عمر خیام‎ ’omar-e khayyām ; * mnamo 1048 mjini Nishapur, mkoa wa Khorasan; † kati ya 1122 - 1131) alikuwa mshairi nchini Uajemi aliyejulikana pia kama mtaalamu wa hisabati, falaki na falsafa.

Kama mwanahisabati aligundua usuluhisho wa milingano ya mchemraba pamoja na kipeo cha mchemraba. Mfalme alimwagiza 1073 kujenga jengo la kuangalia nyota. Akaendelea kutunga kalenda iliykuwa msingi wa kalenda ya jua ya Uajemi inayotumiwa hadi leo na kalenda hii imesifiwa kuwa kamili kushinda kalenda ya Gregori.

Alitunga mashairi aina ya rubaiyat yaliyokuwa na mistari minne kila beti akatunga zaidi ya 1,000. Katika mashairi haya alijadili mawazo yake juu ya falsafa na dini ya Kiislamu.

Alikuwa na elimu nzuri lakini hakupendezwa na Uislamu wa kawaida wa wakati wake. Kati ya mabeti mashuhuri aliyotunga ni

"Furahia divai na wanawake usiogope maana Allah ni mwenye rehema."


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omar Khayyam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.