OC Ukeje

Okechukwu Ukeje, anayejulikana zaidi kwa jina la kisanii OC Ukeje, ni Mnaijeria Muigizaji,[1] Modeli na Mwanamuziki.[2] Alipata umaarufu baada ya kushinda shindano la uhalisia la Amstel Malta Box Office (AMBO).[3] Amejinyakulia tuzo kadhaa ikiwemo Africa Movie Academy Awards, Africa Magic Viewers Choice Awards, Nollywood Movies Awards, Best of Nollywood Awards, Nigeria Entertainment Awards na Golden Icons Academy Movie Awards. Amecheza katika filamu nyingi zilizoshinda tuzo kama vile Two Brides and a Baby, Hoodrush, Alan Poza, Confusion Na Wa na Half of a Yellow Sun.[4]
Maisha ya Awali
[hariri | hariri chanzo]Okechukwu Ukeje, ni mzaliwa wa Umuahia,[5] mji mkuu wa Jimbo la Abia, eneo la kusini mashariki mwa Nigeria. Alizaliwa na kukulia katika Jimbo la Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria. Pia ni mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Adebayo, Tireni (2021-07-16). "OC Ukeje quietly marks 40th birthday". Kemi Filani News (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2022-03-12.
- ↑ I’m Attracted To Older Women – Okechukwu Chukwudi Ukeje 6 Novemba 2012
- ↑ "OC Ukeje, Actor". Mandy. Iliwekwa mnamo 2016-05-13.
- ↑ "List of winners of Nigeria Entertainment Awards 2013".
- ↑ "Why women send nude photographs to me - OC Ukeje". naijanewsmagazine.blogspot.com. 10 Juni 2013.
- ↑ "Nigeria: OC Ukeje, Majid Breaking the Cinemas". allAfrica.com. Iliwekwa mnamo 2016-05-13.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu OC Ukeje kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |