Nenda kwa yaliyomo

Nokia 1100

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simu ya Nokia 1100

Nokia 1100 ni simu madhubuti iliyotengenezwa na Nokia. Imelengewa nchi ambazo bado zinaendelea na watumizi ambao hawahitaji vifaa vingi kwenye simu zao ila ya uwezo wa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi, saa, n.k.

Simu ya 1100 inafanana na Nokia 3210/Nokia 3310 ambazo zilikuwa simu maarufu katika miaka iliyopita kabla ya uzinduzi mpya wa vifaa vya simu kama kamera.

Zaidi ya nakala milioni 200 za simu hii zimeuzwa tangu ilipoanzishwa mnamo 2003, na kuifanya iwe simu iliyopata mauzo mazuri zaidi kote duniani.[1] Hata hivyo, ilishinda mauzo ya Playstation 2 iliyouza nakala milioni 138 na simu ya Motorola RAZR iliyouza nakala milioni 120.).[2]

Yaliyomo

[hariri | hariri chanzo]
  • Simu hii ina taa inayoweza kutumika kama tochi.
  • Kasha yake huweza kubadilidhwa. Kando na kasha lake la buluu, kuna la nyekundu na kijani..[3]
  • Uso wake wa mbele uliundwa kuwa ni wenye kuzuia vumbi.
  • Uwezo wa kubeba ujumbe mfupi 50 kwenye simu yake.[4]

Toleo zingine

[hariri | hariri chanzo]

Kuna simu tano zinazofanana: 1100a, 1100b, 100i, 1101 na 1108.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]