Nokia 3310

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simu ya Nokia 3310

Nokia 3310 ni simu iliyotolewa mnamo 2000. Ilipata mafaniki mazuri kote duniani, kwani iliuza nakala milioni 126.[1] Toleo zingine zinazofanana na 3310 zimetolewa, zikiwemo Nokia 3315, 3320, 3330, 3350, 3360, 3390 and 3395.

Muundo[hariri | hariri chanzo]

Simu hii ni nzito kidogo, na ina betri yenye uzito wa gramu 115. Ina umbo la mstatili, inayotoshea kwenye mkono wa binadamu na inayobofwa kwa kutumia kidole cha gumba. Kibonyezo cha rangi ya buluu ndiyo inayotumika kuchagua vitu na kibonyezo cha "C" hutumika kuondoa kitu. Kibonyezo cha kuwasha na kuzima simu ni ya rangi nyeusi iliyo kwenye juu ya simu.

Yaliyomo[hariri | hariri chanzo]

Simu hii ina vifaa vingi kama saa, kikumbushio, michezo kama Snake, Pairs II na Space Impact. Simu hii ilijulikana kwa uwezo wake wa kukubali utungaji wa ujumbe mfupi iliyo mrefu.

Kasha la simu hii inaweza kubadilishwa. Pia, ilikuwa na zaidi ya milio 35 ya simu.

Toleo zingine[hariri | hariri chanzo]

3315, 3390 na 3395[hariri | hariri chanzo]

Toleo jipya la 3310 ni Nokia 3315 iliyo na:

  • Uwezo wa kuhariri picha
  • Uwezo wa kutumia wimbo wa simu iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi.
  • Vibonyezo vyenye muundo wa njugu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-09-11. Iliwekwa mnamo 2010-01-29.