Nenda kwa yaliyomo

Nicolas Sarkozy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sarkozy tar. 16 Mei 2007 alipokuwa rais

Nicolas Sarkozy (kwa jina kamili Nicolas Paul Stéphane Sarközy de Nagy-Bocsa; * 28 Januari 1955 Paris) ni mwanasiasa aliyekuwa Rais wa Ufaransa tangu 16 Mei 2007.

Sarkozy ni mtoto wa baba mkimbizi kutoka Hungaria na mama wa asili ya Kiyahudi. Alijiunga na siasa akawa mwenyekiti wa chama cha UMP cha rais Jacques Chirac akateuliwa kuwa mgombea wa chama hiki.

Chini ya rais Chirc akawa waziri wa mambo ya ndani kwa miaka mingi. Akajipatia sifa ya kuwa mkali dhidi ya wageni na wahamiaji waliovunja sheria akidai kuwarudisha katika nchi walipotoka au hata nchi za mababu.

Tangu kuwa rais alishangaza watazamiaji wengi kwa kuingiza mawaziri kutoka chama cha upinzani (parti socialiste) katika serikali yake pamoja na mawaziri wenye asili ya Kiafrika na Kiarabu kati yao Rachida Dati (waziri wa sheria), Fadela Amara (waziri msaidizi wa nyumba na maendeleo ya miji) na Rama Yade (waziri msaidizi wa mambo ya nje kwa haki za binadamu).

Mwezi wa Oktoba 2007 Sarkozy alitangaza talaka na mke wake Cécilia Sarkozy atakayeendelea kulea mtoto wao wa pamoja.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Magazeti

[hariri | hariri chanzo]