Ngoma Iko Huku
Ngoma Iko Huku | ||
---|---|---|
Greatest hits ya Salum Abdallah na Cuban Marimba | ||
Imetolewa | 2000 (miaka ya 1955-1965) | |
Aina | Muziki wa dansi | |
Lebo | Dizim Records |
Ngoma Iko Huku ni jina la kutaja albamu yenye nyimbo mchanganyiko kwa vipindi tofauti ya hayati Salum Abdallah akiwa na Cuban Marimba. Albamu imekusanya vibao vyake vyote ambavyo ni vikali na kuviweka pamoja. Hasa kutoka 1955 hadi 1965 mwaka ambao ndio kifo chake kilitokea. Rekodi hizi zilikusanywa na kampuni ya Kijerumani Dizim Records ili kuenzi kazi za mkongwe huyu. Albamu ilitolewa mwaka wa 2000 ikiwa na nyimbo zipatazo 22. Ufundi aliounesha katika nyimbo hizi unapelekea kuonekana kijana hadi sasa. Hata baada ya miaka kupita tangu kufa kwake, lakini bado hata kwa vijana waliozaliwa baadaye wanaelewa mchango wa Salum Abadallah na kuzisikiliza nyimbo zake kwa kiasi kikubwa.[1] Nyimbo nyingi zilikuwa za mapenzi na ukombozi. Hasa kwa vile miaka ile ya 1960 mwanzoni tungo nyingi zilihusu hamasa ya kuileta Afrika huru. Nyimbo kama Beberu na nyimbo zingine za kusifu juhudi za TANU kwa wakati ule.
Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]Hii ni orodha ya nyimbo zilizopo katika albamu hii.
- Ngoma Iko Huku
- Naumiya
- Ubaya
- Nalia Nalia
- Wanipendeza
- Cuba Chacha
- Ndiyo Hali Ya Dunia
- Kazi Tanzania
- Shemeji Shemeji
- Tanzania Twist
- Sipati Majibu
- Salaam Kwa Jumia
- Wanawake Tanzania
- Kachacha
- Tulime Mashamba
- Bebru
- Kimanzi
- Si Kosa Lako
- Unavanja Utu
- Mpenzi Wee
- Maisha Siyatamani
- Afrika Muye Muye
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Ngoma Iko Huku katika wavuti ya Discogs
- ↑ Salum Abdallah katika DW Swahili. SALUM ABDALLAH ATABAKIA KIJANA MILELE mnamo 28.04.2007