Nesiritide
Nesiritide, inayouzwa kwa jina la chapa Natrecor miongoni mwa mengine, ni dawa iliyotengenezwa kutibu ugonjwa wa moyo kukosa ufanisi ya ghafla (acute decompensated congestive heart failure).[1] Hata hivyo, ushahidi umeshindwa kuonyesha manufaa yake.[2][1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya mshipa.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na shinikizo la chini la damu, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na maumivu ya mgongo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha athari za mzio, matatizo ya figo na kifo.[1] Dawa hii ni aina ya molekuli ambazo zimeundwa kwa njia ya uhandisi wa jeni ya peptidi natriuretic ya aina ya B, ambayo husababisha upanuzi wa mshipa (vasodilatation).[1]
Nesiritide iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2001.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban dola 1,100 za Marekani kwa chupa ya miligramu moja na nusu.[3] Uuzaji wake wa kibiashara; hata hivyo, ulikomeshwa kufikia mwaka wa 2021.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 "Nesiritide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Juni 2020. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)"Nesiritide Monograph for Professionals". Drugs.com. Archived from the original on 22 June 2020. Retrieved 12 November 2021. - ↑ O'Connor CM, Starling RC, Hernandez AF, Armstrong PW, Dickstein K, Hasselblad V, Heizer GM, Komajda M, Massie BM, McMurray JJ, Nieminen MS, Reist CJ, Rouleau JL, Swedberg K, Adams KF, Anker SD, Atar D, Battler A, Botero R, Bohidar NR, Butler J, Clausell N, Corbalán R, Costanzo MR, Dahlstrom U, Deckelbaum LI, Diaz R, Dunlap ME, Ezekowitz JA, Feldman D, Felker GM, Fonarow GC, Gennevois D, Gottlieb SS, Hill JA, Hollander JE, Howlett JG, Hudson MP, Kociol RD, Krum H, Laucevicius A, Levy WC, Méndez GF, Metra M, Mittal S, Oh BH, Pereira NL, Ponikowski P, Tang WH, Wilson WH, Tanomsup S, Teerlink JR, Triposkiadis F, Troughton RW, Voors AA, Whellan DJ, Zannad F, Califf RM (Julai 2011). "Effect of nesiritide in patients with acute decompensated heart failure" (PDF). The New England Journal of Medicine. 365 (1): 32–43. doi:10.1056/NEJMoa1100171. PMID 21732835. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2021-02-11. Iliwekwa mnamo 2021-09-18.
{{cite journal}}
:|hdl-access=
requires|hdl=
(help); Unknown parameter|displayauthors=
ignored (|display-authors=
suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Natrecor Prices, Coupons & Patient Assistance Programs". Drugs.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Drugs@FDA: FDA-Approved Drugs". www.accessdata.fda.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 12 Novemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nesiritide kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |