Neshani Andreas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Neshani Andreas
Amezaliwa 1964
Walvis Bay, Namibia
Amekufa May 2011
Windhoek, Namibia
Nchi Namibia
Kazi yake Mwandishi na Mwalimu


Neshani Andreas (1964 - Mei 2011) alikuwa mwandishi wa Namibia, ambaye pia alifanya kazi kama mwalimu kutumikia kikosi cha kijeshi cha Amerika kiitwacho (Peace Corps).[1] Anajulukana zaidi kwa riwaya yake ya The Purple Violet of Oshaantu, ambayo ilimfanya awe mtu wa kwanza wa Namibia kuwemo katika safu ya Waandishi wa Kiafrika ya Heinemann.[2][3][4] Alifariki akiwa na umri wa miaka 46, baada ya kupatikana na saratani ya mapafu mwanzoni mwa mwaka 2010.[4][5]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa huko Walvis Bay, Kusini-Magharibi mwa Afrika (sasa Namibia), mwaka 1964, akiwa ni wa pili kati ya watoto nane, na kazi yake ya kwanza alifanya katika kiwanda cha mavazi. Wazazi wake wote wawili walikuwa wafanyakazi katika kiwanda cha samaki. Tangu akiwa mdogo, Andreas alitaka kuwa mwandishi.Alisoma katika chuo cha uwalimu huko Ongwediva na alifundisha hapo kwa miaka mitano. Baadaye, Andreas alisomea Shahada ya Sanaa na diploma ya uzamili ya elimu katika Chuo Kikuu cha Namibia.[6] Alikuwa mkurugenzi msaidizi wa kikosi cha kijeshi kiitwacho Peace Corps cha Marekani nchini Namibia kwa miaka minne. Ni hapo alipo kutana na mtu wa kwanza kumhimiza kuandika, ambapo baadaye alisema kuwa ni moja ya nyakati zenye thamani zaidi katika maisha yake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neshani Andreas kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Neshani Andreas – Namibian Author for Women's Rights". The Namibian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-05-28. 
  2. "Purple Violet of Oshaantu, The - Weaver Press". weaverpresszimbabwe.com. Iliwekwa mnamo 2022-05-28. 
  3. Andreas, Neshani (2004). The purple violet of Oshaantu. Avondale, Harare: Weaver Press. ISBN 1-77922-035-9. OCLC 64427146. 
  4. 4.0 4.1 "Namibia: Neshani Andreas - A Gallant Local Author (1964-2011)". Iliwekwa mnamo 2022-05-28. 
  5. "Namibia: Local Author Neshani Andreas Dead". Iliwekwa mnamo 2022-05-28. 
  6. "Neshani Andreas: a passion for writing. - Free Online Library". www.thefreelibrary.com. Iliwekwa mnamo 2022-05-28.