Neema Decoras

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Neema Decoras
Neema Decoras
Neema Decoras
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Neema Benard Decoras
Amezaliwa 27 Julai 1984 (1984-07-27) (umri 35)
Mbeya, Tanzania
Asili yake Mbeya, Tanzania
Aina ya muziki Gospel
Kazi yake Mwimbaji, Mtunzi wa nyimbo
Ala Sauti
Aina ya sauti Soprano
Miaka ya kazi 2012-hadi leo
Studio Twins Records (2012)
Amba Records (2013–Hadi leo)
Tovuti www.neemadecoras.com

Neema Decoras (Amezaliwa Tarehe 27 Julai 1984) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo za Injili za Kikristo mwenye kipawa na hodari kutoka nchini Tanzania ambaye amejitoa kuwa chombo imara cha Uinjilisti na kutumikia kusudi la Mungu katika wakati wake. Alizaliwa katika jiji la Mbeya, Tanzania na ni watatu kuzaliwa katika familia ya watoto saba.

Neema Decoras ambaye kwa sasa ni mama wa watoto wawili wa kike na mke mpendwa wa mume mmoja alianza uimbaji wa nyimbo za injili akiwa mdogo sana katika shule ya Jumapili ya Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT) kabla ya kuokoka na kubatizwa na mchungaji Mwakanyamale wa Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) ya Ilembo, Airport, Mbeya.

Neema Decoras aliendelea na huduma ya uimbaji katika kipindi chote alichokuwa akisoma, kuanzia shule ya msingi hadi sekondari. Akiwa anachukua elimu ya sekondari alikuwa mwanachama na mwalimu wa kwaya ya Christ's Ambassadors Students Fellowship Tanzania (CASFETA) katika shule yake na muimbaji wa nyimbo za kusifu na kuabudu katika kikundi cha kusifu na kuabudu na Kwaya ya Tumaini ya Kanisa La Pentekoste Tanzania (KLPT). Ni katika kipindi hicho ndipo alipoanza kuwa na haja ya kukitumia kipawa cha uimbaji na utunzi wa nyimbo na kufanya huduma ya uimbaji kama muimbaji wa kujitegemea.

Haja ya kuwa muimbaji wa kujitegemea ilianza kutimia mwishoni mwa mwaka wa 2012 Neema Decoras alipofanikiwa kurekodi wimbo wake uitwao “Mungu ni Mwema” katika studio iitwayo Twins Records iliyopo Riverside, Ubungo jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji wa muziki aitwaye Gabriel Maulana.

Mnamo January mwaka wa 2013 mume wake alimpeleka kwa mtayarishaji wa muziki aitwaye Ambangile Mbwanji anayejulikana sana kama Amba ambaye ni mmiliki wa studio iitwayo Amba Records iliyoko Ukonga, Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Katika studio hiyo alifanikiwa kurekodi na kutoa albamu yake ya kwanza mwezi Julai mwaka wa 2013. Albamu hiyo iitwayo “Milele Nitalisifu Jina Lako” ina nyimbo nane ambazo zote ameziimba kwa lugha ya Kiswahili. Nyimbo zilizomo katika albamu hiyo ni; Milele Nitalisifu Jina Lako, Mikononi mwa Mungu, Unapojaribiwa, Nione Leo, Mungu ni Mwema, Rejea kwa Yesu, Ninaimba Sifa na Hakika Nimejua.

Akiongozwa na Neno kutoka katika Zaburi 145:1-2 “Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi Jina lako milele na milele. Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu Jina Lako Milele na Milele” Neema Decoras anasema kamwe hawezi kuacha kulisifu Jina la Bwana kwa kuwa Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana.

Kwa sasa Neema Decoras anaishi jijini Dar es Salaam ambapo amefanya maonyesho yake mengi sana japo yuko tayari kutumika katika Ibada, Matamasha na Mikutano ya Injili, Semina, Sherehe, na matukio mbalimbali ambayo yanahubiri Neno la Mungu popote pale ndani na nje ya Tanzania.

Muziki[hariri | hariri chanzo]

Albamu zake kwa lugha ya Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

Single zake[hariri | hariri chanzo]

Mwaka Single Nafasi iliyoshika
EA CAN U.S. UK FRA
2012 "Mungu ni Mwema" 1 - - - -
2013 "Milele Nitalisifu Jina Lako" 1 - - - -

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]


WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Neema Decoras kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.