Nenda kwa yaliyomo

Ndumbagwe Misayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ndumbagwe Misayo (Thea))
Ndumbagwe Misayo
AmezaliwaNdumbangwe Misayo
UtaifaMtanzania
Kazi yakeMuigizaji, mtayarishaji wa filamu,muongozaji wa filamu,
Miaka ya kazi2000-hadi sasa

Ndumbangwe Misayo (maarufu kama “Thea”; alizaliwa katika mkoani Shinyanga. mwaka 1982) ni msanii katika tasnia ya uigizaji wa filamu za kitanzania.

Ni mtoto wa kwanza katika familia ya Gaudence Urassa na Matilda Misayo. Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Mapambano iliyopo Sinza na baadaye kujiunga na sekondari ya Zanaki aliposoma mpaka kidato cha tatu kisha kuhamia shule ya sekondari Green Victoria alipohitimu kidato cha nne mwaka 2001.[1]

Sanaa ya uigizaji alianza tangu shule ya msingi alipokuwa darasa la tano katika kikundi cha sanaa cha shule na pia katika Kanisa Katoliki la Mwananyamala ambapo napo alihusika katika maigizo mbalimbali pale parokiani. Alipoanza kidato cha kwanza alijiunga na kikundi cha sanaa cha Mambo hayo ambacho baada ya muda kilivunjika akahamia katika kikundi cha Kaole ambapo igizo la mwisho kucheza hapo Kaole lilikuwa ni “Baragumu” mwaka 2005.

Alipokea tuzo ya mwigizaji bora wa kike mwaka 2008.

Filamu alizoshiriki

[hariri | hariri chanzo]
  • Malaika wangu
  • Bibi yangu
  • Sindano ya moto
  • Pasuko la moyo
  • Think before
  • Mnyororo
  • Kovu la laana
  • Mtoto wa mbwa
  • Cheque in the bible
  • She is mine
  • Chaguo langu
  • Saa 4
  • My wife
  • Sorry my son
  • Impossible promise
  • Because of you
  • Tension of love
  • Ray of hope
  • Solemba
  • The perfect man
  • Lonely heart
  • Mtoto wa kitaa
  • Not without my son
  • Moses
  • Young billionaire
  • Power of God
  • Fantasy
  • Bed rest
  • Dadaz
  • The cellular
  • Love is war
  • Ukungu
  • Trip to America
  • Suspense
  • Kiapo cha damu
  • Inspector Seba
  • Roho sita
  • Sikitiko langu
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndumbagwe Misayo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-11-05. Iliwekwa mnamo 2018-12-01.