Navi Pillay
Navanethem "Navi" Pillay (alizaliwa Durban, jimbo la Natal, 23 Septemba 1941) ni wakili kutoka nchini Afrika Kusini aliye maarufu kwa kazi yake huko Umoja wa Mataifa.
Alizaliwa familia maskini yenye asili ya Tamil, India. Baba yake alikuwa dereva wa basi. Navi ameolewa na mwanasheria Gaby Pillay mnamo mwezi Januari mwaka wa 1965. Kwa pamoja wana watoto wawili pamoja.[1] Navi alikuwa mwanamke wa kwanza asiye-mzungu kushika wadhifa wa jaji mkuu wa mahakama Afrika Kusini.
Pillay alisoma katika chuo kikuu cha Natal na alijiunga na masomo ya shahada ya sanaa mwaka 1963 na kumaliza 1965. Baadaye, alienda kujiendeleza kimasomo huko Chuo Kikuu cha Harvard. Huko nako alihitimu shahada ya pili ya sheria, LLM, mnamo mwaka wa 1982—vilevile daktari wa shahada ya ujuzi wa sayansi kunako mwaka wa 1989.
Kazi ya Uwakili
[hariri | hariri chanzo]Katika mwaka 1967, Pillay alianzisha kampuni yake ya Uwakili kwa sababu yeye hakuweza kufanya kazi katika kampuni yoyote ya uwakili wakati wa ubaguzi wa rangi.[2] Yeye alifanya kazi katika kampuni ya uwakili kwa miaka ishirini na nane. Yeye alisaidia wanaharakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi. Katika mwaka 1992, Pillay alianzisha shirika la Equality Now kwa ajili ya kusaidia wanawake.[3]
Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
[hariri | hariri chanzo]Katika mwaka 1995, Nelson Mandela alimteua Pillay kuwa jaji wa mahakama ya juu ya Afrika Kusini. Yeye alikuwa mwanamke wa kwanza wa rangi kuteuliwa kuwa jaji wa mahakama ya juu ya Afrika Kusini. Baadaye kidogo, Umoja wa Mataifa ulimteua kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.[4]
Yeye alikuwa katika mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya rwanda kwa miaka nane. Yeye alikuwa rais wa mahakama hiyo kwa miaka minne. Katika mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya rwanda, Pillay na majaji wengine walisababisha ubakaji kujulikana kama silaha ya mauaji ya kimbari. Walifanya hivyo baada ya Pillay kuuliza mashahidi mmoja mmoja shahidi kuhusu uzoefu wao. Uamuzi huu ulikuwa wa mara ya kwanza kwa ubakaji kuonekana kuwa silaha ya vita.[5]
Baada ya mahakama ya kimataifa ya mauaji ya kimbari ya rwanda, Pillay aliteuliwe kwa mahakama ya kimataifa ya jinai katika mwaka 2006. Alihudumu kwa miaka sita. Kisha yeye aliteuliwe kama kamishna mkuu wa haki za binadamu. Alihudumu kwa miaka nane hadi mwaka 2008 hadi 2014. Yeye aliunga mkono haki za mashoga kama kamishna mkuu wa haki za binadamu. Sasa, yeye ni Kamishna wa Tume ya Kimataifa dhidi ya Adhabu ya Kifo.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Navi Pillay", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2019-06-25, iliwekwa mnamo 2019-07-25
- ↑ Profile: New UN human rights chief (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2008-07-28, iliwekwa mnamo 2019-07-25
- ↑ "Equality Now". Equality Now (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Home | United Nations International Criminal Tribunal for Rwanda". unictr.irmct.org. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
- ↑ "Wayback Machine" (PDF). web.archive.org. 2014-01-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-01-03. Iliwekwa mnamo 2019-07-25.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Navi Pillay kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |