Nasalsa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nasalsa alikuwa malkia wa Nubia wa Ufalme wa Kush. Anajulikana kutokana na shabti, baadhi ya maandishi kwenye vitabu vidogo na vikombe, maandishi kwenye stela ya Khaliut, maandishi ya kutolewa na maandishi kutoka Kawa.[1] Dodson anataja kwamba Nasalsa anatajwa kwenye stela ya Kutawazwa kwa Atlanersa na kwenye stela za Uchaguzi na Uteuzi wa Aspelta. Stela hizi zilitoka Gebel Barkal.[2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Nasalsa alikuwa binti wa Atlanersa, mke-ndugu wa Senkamanisken, na mama wa wafalme Anlamani na Aspelta pamoja na malkia Madiqen.[1][2] Stela ya Anlamani (Kawa VIII) ina sehemu inayoelezea Nasalsa akiitwa na kumpata mwanae kwenye kiti cha enzi. Sasa mama wa mfalme Nasalsa aishi milele, alikuwa miongoni mwa dada wa kifalme. Mama wa mfalme, mpenzi wa upendo, alikuwa malkia wa wake wote. Mfalme alituma marafiki ili aletwe. Alikuta mwanae akiwa kama Horus kwenye kiti chake cha enzi. Alikuwa na furaha sana baada ya kuona uzuri wa Mfalme.[3]

Stela ya Uteuzi wa Aspelta inamrejelea Nasalsa kama Dada wa Mfalme, Mama wa Mfalme, Malkia wa Ufalme wa Kush, na Binti wa Re. Maandishi yanasema kuwa Nasalsa alikuwa binti wa Dada wa Mfalme, Mhudumu wa Amen-Re huko Thebes, Misri Amenirdis II. Uhusiano huu labda ulikuwa kupitia ulezi, kwa sababu Mhudumu huko Thebes aliaminiwa kuwa mtawa. Kutajwa kwa Binti wa Re ilikuwa mara ya kwanza malkia wa Kush kutumia cheo hicho.[4]

Stela ya Chaliut kutoka Gebel Barkal B500 inamuelezea Nasalsa akiwa kama Isis alivyokuwa na Horus wakati inaposema kuwa Aspelta alikuwa kwenye kiti cha enzi cha Horus.[5] Hii inaweza maanisha kuwa Nasalsa alikuwa msimamizi wa kifalme au mwenzake katika utawala.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Dows Dunham, M. F. Laming Macadam: Names and Relationships of the Royal Family of Napata, Journal of Egyptian Archaeology. 35, 1949, pp.142 (Plate XVI; nr 50), 145
  2. 2.0 2.1 Aidan Dodson & Dyan Hilton: The Complete Royal Families of Ancient Egypt. Thames & Hudson, 2004, pp 236-37, 239 ISBN 0-500-05128-3
  3. Roberto B. Gozzoli, Kawa V and Taharqo's byȜwt: Some Aspects of Nubian Royal Ideology, The Journal of Egyptian Archaeology, Vol. 95 (2009), pp. 235-248, JSTOR
  4. B. G. Haycock, The Kingship of Cush in the Sudan, Comparative Studies in Society and History, Vol. 7, No. 4 (Jul., 1965), pp. 469-470, 477, Cambridge University Press, JSTOR
  5. 5.0 5.1 Joyce Haynes; Mimi Santini-Ritt (2012). "Women in Ancient Nubia". Katika Marjorie M. Fisher; Peter Lacovara; Salma Ikram n.k. Ancient Nubia: African Kingdoms on the Nile. The American University in Cairo Press. uk. 173. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nasalsa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.