Nenda kwa yaliyomo

Isis

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuhusu kundi la kigaidi linaloitwa ISIS, angalia Daish

Isis

Isis alikuwa mmoja wa miungu katika dini ya Misri ya Kale. Alikuwa mungu wa kike aliyeabudiwa na Wamisri wengi katika maisha ya kila siiku kwa sababu aliaminiwa kuhusika na shughuli za uzazi na kujifungua, na kutoka hapa maombi mengi ya uponyaji yalilengwa kwake.

Kama mungu wa uhai na uchawi, Isis aliwalinda wanawake na watoto, na kuwaponya wagonjwa. Alitazamiwa kama mama wa kimungu wa kila farao (mfalme).

Katika mitholojia ya Misri aliunganishwa hasa na Osiris (mume wake wa kimungu) na Horus (mwana wa Osiris na Isis). Ibada ya Isis iliendelea muda mrefu hadi kipindi cha utawala wa Kiroma, ikaenea pia nje ya Misri katika Dola la Roma.

Alama zake zilikuwa ankh, mabawa yake, na taji lilionyesha kiti cha kifalme.

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

  • Richard H. Wilkinson: The complete gods and goddesses of ancient Egypt], Thames & Hudson (2003), ISBN 978-0-500-05120-7
  • Gods and Goddesses of Ancient Egypt by Janeen R, Adil

Tovuti zingine[hariri | hariri chanzo]