Nancy Khedouri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nancy Dinah Elly Khedouri ni mwanasiasa, mfanyabiashara na mwandishi wa Bahrain. Amekuwa akihudumu kwenye bunge la Bahrain tangu mwaka 2010.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Familia Khedouri ni kati ya familia za Kiyahudi, ni familia inayoingiza bidhaa kama vitambaa kutoka nje. Yeye ni kizazi cha tatu, na binamu yake Houda Nonoo, balozi wa Bahrain nchini Marekani kuanzia 2008 hadi 2013.

Kwenye kitabu chake alichokiandika mwaka 2007 aliandika historia ya Wayahudi nchini Bahrain.

Mwaka 2010 alichaguliwa kama mbunge. Amekuwa akifanya kazi ya kudumisha mahusiano mazuri na wananchi wa Kiyahudi, alijitokeza hadharani akiwa na viongozi wa Kiyahudi na kisiasa kama Yisrael Katz. Aliwakilisha nchi katika kongamano la dunia la Wayahudi.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nancy Khedouri kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.