Nenda kwa yaliyomo

Houda Nonoo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Nonoo 2008-07-28

Houda Ezra Ebrahim Nonoo (alizaliwa Manama, 7 Septemba 1964) alihudumu kama balozi wa Bahrain nchini Marekani kutoka mwaka 2008 hadi 2013. Aliteuliwa kwa mamlaka ya waziri wa mambo ya nje Khaled Ben Ahmad Al-Khalifa[1]. Alikuwa Myahudi wa kwanza na mwanamke wa tatu kuteuliwa kama balozi wa Bahrain. Alikuwa balozi wa wayahudi kwa nchi za kiarabu na mwanamke wa kwanza kuwa balozi wa Bahrain nchini Marekani.[2][3][4][5]

Nonoo alizaliwa kwenye familia ya Wayahudi ambao ni wafanyabiashara wenye asili ya Iraki. Babu yake aliondoka Baghdad na kuhamia Bahrain alikoanzisha biashara ya fedha. Aliishi kwa muda mrefu nchini Uingereza alikopata elimu yake ya chuo Carmel, shule ya kiahudi[6] alihitimu stashahada ya masomo ya biashara na kisha alifunga ndoa na Salman Idafar ,aliyekuwa na asili ya uyahudi na uingereza na walipata watoto wawili Manasheh na Ezra.Baba yake alipofariki kwenye ajali alirejea nchini Bahrain ili kuiendeleza kampuni iliochwa na baba yake, kampuni iliyokuwa ikitoa huduma za kitekinologia, usafi na kadhalika na alifanikiwa kuwa mfanyabiashara mashuhuri baada ya kurithi kampuni hiyo.

Kabla ya kuteuliwa kwenye taasisi ya Majlis al-shura mwaka 2005[7][8] [2][3][9] .Mwaka 2004 alianzisha chama cha maswala ya haki za binadamu cha Bahrain na kilikuwa ni chama kilichokuwa kinasaidia kusimamia haki na maendeleo ya wanawake na wafanyakazi wa kigeni nchini Bahrain.Kwa miaka mitatu alihudumu kama mbunge, baada ya kuteuliwa na mfalme Hamad ibn Isa Al Khalifah. Uteuzi wake ulizungumziwa kwasababu Huoda alikuwa ni sehemu wa jumuia ndogo ya wahudi nchini Bahrain iliyoundwa na watu 37 na wengi wakiwa ni vizazi vya kutoka Irani na Iraki.Yeye siyo wa kwanza kutoka jumuiya hiyo kuteuliwa kama mtumishi wa serikali, babu yake Abraham Nonoo aliteuliwa kama mmoja wa watumishi halimashauri ya Manama na ndio aliyekuwa mtu wa kwanza kuteuliwa na halimashauri hiyo.Mwaka 2000 binamu yake Ebrahim Daoud Nonoo aliteuliwa kama kuhudumu katika bunge.

Uteuzi kama balozi wa Marekani

[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 3 Julai mwaka 2008 , aliteuliwa kama balozi wa ufalme wa Bahrain nchini Marekani [10] , akiwa amepewa majukumu ya kidiplomasia kwa nchi kama Kanada , Meksiko ,Brazili na Ajentina .Baadhi ya vyombo vya habari vya ndani vilipinga uteuzi wake na radio moja nchini Kanada ilisema kuwa myahudi hawezi kuwa mtetezi wa nchi ya Bahrain. Mfalme Al-Khalifa aliipuuza taarifa hizo.[2]

Akiwa balozi alifanya mabadiliko kama kubadilisha mijumuiko ya futari kutoka kwa wanaume tupu hadi kuwa na mchanganyiko na wanawake kisha watu wa dini na dhehebu mbalimbali

Muda wake wa utumishi kama balozi uliisha 2013 na nafasi hiyo ilichukuliwa na Abdullah bin Mohammad bin Rashed Al Khalif.[11]

 1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-23. Iliwekwa mnamo 2021-07-23.
 2. 2.0 2.1 2.2 "Bahreïn persiste et signe", Radio Canada, June 8, 2008
 3. 3.0 3.1 "Une juive ambassadrice d'un pays arabe", Radio Canada, May 31, 2008
 4. "Bahrain names Jewish ambassador". BBC News. 2008-05-30. Iliwekwa mnamo 2008-05-30.
 5. "Bahraini king taps Jewish woman lawmaker as envoy to U.S." Haaretz. 2008-06-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-05-06. Iliwekwa mnamo 2008-05-29. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
 6. {{cite news|date= 4 December 2008|access-date = 6 May 2020|author= Round, Simon|url=https://www.thejc.com/lifestyle/interviews/interview-houda-nonoo-1.6547%7Ctitle= Archived 22 Oktoba 2021 at the Wayback Machine. Interview: Houda Nonoo|work= The Jewish Chronicle
 7. Houda Nonoo Archived 2016-08-21 at the Wayback Machine. Wise Muslim Women - Women of other Faiths
 8. "Arab Spring, Israel and Bahrain's 38 Jews in the eyes of Jewish ambassador to U.S." Jewish News Service. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2016-07-16. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)
 9. Nancy Elly Khedourie, From Our Beginning to Present Day (Al Manar Press: 2007) p. 78
 10. "Bahrain picks Jew as U.S. envoy, local media critical". Reuters. 2008-05-08. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2010-10-27. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help); Unknown parameter |= ignored (help)
 11. Chief, Habib Toumi, Bureau (15 Novemba 2013). "Bahrain appoints new ambassador in Washington".{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link)