Najla Bouden

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Waziri Mkuu wa Tunisia aliye madarakani
Waziri Mkuu wa Tunisia aliye madarakani

Najla Bouden (pia anajulikana kama Najla Bouden Romdhane; alizaliwa 29 Juni 1958) ni mwanajiolojia na profesa wa chuo kikuu wa Tunisia ambaye anahudumu kama Waziri Mkuu wa Tunisia. Alichukua madaraka tarehe 11 Oktoba 2021, na kumfanya kuwa waziri mkuu wa kwanza mwanamke nchini Tunisia na ulimwengu wa Kiarabu. [1] Hapo awali alihudumu kwenye wizara ya elimu mwaka 2011. [2]

Maisha ya mapema na kazi[hariri | hariri chanzo]

Bouden alizaliwa mwaka wa 1958 huko Kairouan . Yeye ni mhandisi kitaaluma na profesa wa elimu ya juu wa Shule ya Kitaifa ya Uhandisi ya Tunis ya Chuo Kikuu cha Tunis El Manar, na amebobea kwenye jiosayansi. [3] Ana Shahada ya Uzamivu ya(Ph.D.) kutoka École des Mines de Paris katika uhandisi wa tetemeko la ardhi . Kazi yake imezingatia hathari za mitetemo huko Tunis . [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Najla Bouden kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.