Nenda kwa yaliyomo

Naisula Josephine Lesuuda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Naisula Josephine Lesuuda (alizaliwa Samburu, 30 Aprili 1984[1] ) ni mwanasiasa na mwanaharakati wa haki za wanawake wa Kenya. Pia ni Mbunge wa Bunge la Kenya.

Maisha ya Awali[hariri | hariri chanzo]

Lesuuda alizaliwa ni mtoto wa kwanza kati ya watatu kwa mama yao ambaye ni askofu wa Kianglikana na mfanyabiashara.[2]Alihitimu shahada ya mawasiliano na maendeleo ya jamii kutoka Chuo Kikuu cha Daystar.[3]

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Lesuuda alifanya kazi kama mwandishi wa habari katika Shirika la Utangazaji la Kenya, ikiwa ni pamoja na kuandaa na kuendesha kipindi cha Good Morning Kenya yaani Habari ya asubuhi Kenya.[4] Mnamo 2009, baada ya watu kumi kuuawa katika wizi wa mifugo huko Laikipia, alikua mwanachama mwanzilishi wa Msafara wa Amani wa Laikipia. [5]Hili nalo lilipelekea kuanzishwa kwa idadi ya mashirika mengine ya amani ya ndani, yanayoungwa mkono na serikali ya Kenya na Marekani (USAid). Mnamo 2010, kazi yake na shirika hili ilimpelekea kuwa mwanamke mdogo zaidi wa Kenya kushinda Tuzo ya urais ya Grand Warrior.[6] [7]

Mnamo 2013, Lesuuda aliacha kazi yake na kuanzisha "Naisula Lesuuda Peace Foundation" ambayo inatetea elimu ya wasichana na kutokomeza ukeketaji na ndoa za utotoni.[8]

Lesuuda alishiriki katika kampeni ya Rais Uhuru Kenyatta mwaka wa 2013,[9]na kisha kuteuliwa kwa tiketi ya chama chake cha TNA kuwakilisha Kaunti ya Samburu katika Seneti mwaka wa 2013, na kuwa mwanachama mdogo zaidi wa kike.[10] Kisha alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Wanawake wa Kenya.

Mnamo 2016, alitangaza kwamba angeondoka kwenye Seneti kutafuta kuchaguliwa kama mwanachama wa Bunge la Kitaifa la Samburu Magharibi, kisha mwaka wa 2017 akihama kutoka Jubilee hadi chama cha KANU.[11]

Katika uchaguzi wa 2017, Lesuuda alichaguliwa kwa kura 14,560, akimshinda Jonathan Lelelit aliyemaliza muda wake aliyepata kura 13,970,[12] na kuwa mbunge wa kwanza mwanamke katika eneo/jimbo hilo. Bunge lilipoketi mnamo Agosti 2017, alitangaza nia yake ya kuomba nafasi ya Naibu Spika, lakini akashindwa kuwasilisha ombi lake kabla ya kupiga kura.[13]

Alichaguliwa tena katika Eneo la Bunge la Samburu Magharibi katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Lesuuda ameolewa, na ana mabinti wawili.[14]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-27. Iliwekwa mnamo 2024-06-19.
  2. https://www.kenya-today.com/revelations-dennis-itumbi-exposed-badly-by-activist-boniface-mwangi/
  3. https://www.standardmedia.co.ke/article/2000058109/her-cause-captured-kibaki-s-eye
  4. https://www.forbes.com/sites/mfonobongnsehe/2014/12/04/the-20-youngest-power-women-in-africa-2014/#282437955895
  5. https://books.google.co.tz/books?id=5W2VgDhWPqoC&redir_esc=y
  6. https://www.standardmedia.co.ke/article/2000058109/her-cause-captured-kibaki-s-eye
  7. https://www.konnectafrica.net/naisula-lesuuda/
  8. https://leadingladiesafrica.org/
  9. https://www.kenyans.co.ke/news/senator-naisula-lesuuda-defects-jubilee-kanu-she-vies-samburu-west-mp-17427
  10. https://nation.africa/kenya/news/politics/Nominated-women-senators/1064-3991866-xypbkhz/index.html
  11. https://www.the-star.co.ke/news/2017-03-12-senator-naisula-lesuuda-ditches-jubilee-for-kanu/
  12. https://www.the-star.co.ke/news/2017/08/10/video-lesuuda-floors-heavyweight-lelelit-in-samburu-west-mp-race_c1613954
  13. https://www.the-star.co.ke/news/2017/08/25/lesuuda-guns-for-deputy-speaker-seat-as-parliament-opens_c1623689
  14. https://www.tuko.co.ke/234158-kenyans-explode-murkomen-lesuda-love-affair-exposed.html