Muundo wa insha
Mandhari
Muundo wa insha una sehemu nne zifuatazo:
- 1. Kichwa cha insha: kichwa cha insha hudokeza kile unachotaka kukijadili katika insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k.
- 2. Utangulizi: Mambo yaliyomo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.
- 3. Kiini cha insha: katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako; maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
- 4. Hitimisho: hapa ndipo pana muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichojadiliwa katika insha.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muundo wa insha kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |