Musa Otieno
Musa Otieno (alizaliwa Nairobi, 29 Desemba 1973) ni Mkenya anayecheza soka ambaye kwa sasa anachezea kilabu cha Santos katika Ligi kuu ya Premier Soccer League ya Afrika Kusini.
Uchezaji wake
[hariri | hariri chanzo]Kilabu
[hariri | hariri chanzo]Otieno amefurahia uchezaji katika bara lake, amechezea timu za AFC Leopards na Tusker FC za Kenya, na tangu mwaka wa 1997 , Santos katika ligi ya Afrika Kusini ya Premier Soccer League. Ameichezea zaidi ya mechi 300 na kufiungia mabao zaidi ya 30 , na kuwasaidia kushinda makombe ya PSL Championship mwaka wa 2001/02, Bob Save Super Bowl mwaka wa 2001,BP Top 8 mwaka wa 2002, na Kombe la ABSA mwaka wa 2003. Aliteuliwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini mwaka wa 2007.
Otieno alikwenda Marekani mara ya kwanza mwaka wa 2008, alikochezea Cleveland City Stars kwenye ligi ya Divisheni ya Pili ya USL akiwa kwa mkopo kwa msimu mmoja. Alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Stars tarehe julai 4, 2008, kama mchezaji wa akiba dakika ya 64 alipoingia mahala pa Marko Schulte, na baadaye k kushinda taji la ligi ya USL2.
Tarehe 15 Desemba 2008, baada ya hitimisho ya msimu wa ligi ya nyumbani ya Santos , Otieno alirejea Cleveland City Stars ambako alicheza kwenye msimu wao katika ligi ya Divissheni ya Kwanza ya USL mwaka wa 2009 [1]
Kimataifa
[hariri | hariri chanzo]Otieno ni mojawapo wa wachezaji mashuhura walioheshimika nchini Kenya ,kwani aliichezea timu ya taifa ya Kenya kwa mara ya kwanza dhidi ya Zaire mwaka wa 1993 akiwa tu na umri wa miaka 19. Tangia hapo,amekuwa nahodha wa Harambee Stars mara kadhaa. Alikuwa pia miongoni mwa kikosi cha timu ya Kenya cha mwaka wa 2004 kwenye Kombe la Mataifa ya Bara Afrika, ambao walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi lao katika mzunguko wa kwanza wa ushindani, na hiv basi kushindwa kufuzu kwa robo fainali.
Anakisiwa kuichezea timu ya taifa ya Kenya [2] zaidi ya mechi 100 lakini madai haya hayajawahi kudhibitishwa.
Maisha ya binafsi
[hariri | hariri chanzo]Otieno anamiliki na kuendesha shirika la kusaidia jamii nchini mwake, liitwalo Musa Otieno Foundation.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- http://usl1.uslsoccer.com/home/295095.html Ilihifadhiwa 31 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.
- http://www.musaotienofoundation.org/ Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu Mchezaji Soka wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Musa Otieno kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |