Nenda kwa yaliyomo

Munshi Premchand

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Dhanpat Rai Srivastava

Munshi Premchand (Kihindi: प्रेमचंद premchand; 31 Julai 1880 - 8 Oktoba 1936) alikuwa kati ya waandishi muhimu wa fasihi ya Kihindi ya kisasa.

Alizaliwa kama mtoto wa mtumishi wa Posta ya Uhindi ya Kiingereza katika kijiji kidogo karibu na mji wa Varanasi. Mamake alikufa wakati bado alikuwa mdogo naye baba alifariki alipokuwa mwanafunzi wa miaka 14. Hivyo alibaki na kazi ya kulisha wadogo zake akapata riziki kidogo kama mwalimu wa nyumbani.

1898 alipita mtihani akawa mwalimu wa serikali wakati alipoendelea kusoma jioni na kutimiza kiwango cha B.A. Kwa muda aliendelea kama mtumishi wa serikali hadi kujipattia maisha kutokana na vitabu vyake lakini alibaki mtu maskini maisha yote.

Upande wa maisha ya binafsi aliozwa kufuatana na desturi ya Kihindu alipokuwa na miaka 15 tu. Ndoa hii iliharibika na baadaye akamwoa mjane tendo ambalo halikukubaliwa verma kijamii wakati wake lakini kwake ilikuwa ndoa nzuri.

Premchand aliandika mengi kwa lugha ya kawaida iliyoeleweka vizuri kwa watu wengi. Akatunga masimulizi mafupi 300 pamoja na riwaya mbalimbali zinazosimulia maisha ya watu wa kawaida.

"Godaan" (Zawadi ya ng'ombe) ilikuwa riwaya yake ya mwisho. Mkulima maskini Hori anaota ndoto kuwa na ng'ombe mmoja kwa sababu ni ishara ya utajiri katika kijiji cha Kihindi. Anafaulu kujipatia mmoja lakini malipo yake ni maisha. Baada ya kifo chake kasisi wa kjiji anadai ngòmbe kutoka mjane wake kama sadaka kwa raha ya roho yake.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]