Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Muddyb/Patrick Komu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Patrick Peter Zacharia Komu (17 Disemba 2010 - 3 Julai 2018) alikuwa mwanamitindo aliyejizolea umaarufu kama mchungaji mtoto kutoka nchini Tanzania. Huyu ni mtoto wa Rose Alphonce maarufu kama Muna Love, sahib wa karibu wa zamani wa Wema Sepetu na Elizabeth Michael. Mtoto huyu alipenda sana kutoa neno la Mungu na mara kadhaa ameonekana kurejea maandiko matakatifu katika posti nyingi zilizosambaa katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania. Umaarufu wake umekuja baada ya mama yake kuonekana kuambatana nae mara kwa mara katika shughuli mbalimbali.

Baada ya kuwa Mlokole, mtoto aliendelea kueneza dawa kwa vijana wenzake na watu wazima. Bandiko nyingi za Instagrama zinamwonesha akifanya makemezi dhidi ya machafu. Alikuja kuingia katika gumzo kubwa mtoto huyu baada ya kuanza kuugua na kupelekwa jijini Nairobi, Kenya. Hakukaa sana, akapoteza maisha. Kukawa na mikingamo ya baba halali wa mtoto Patrick. Jambo hilo lilizua cheche kubwa katika mitandao ya kijamii nchini Tanzania, huku lawama na maneno mengi mabaya yakielekezwa kwa mama wa mtoto. Awali alionekana Casto mtangazaji wa Clouds TV wa kipindi cha Sizi Kitaa kuonekana kujinadi kuwa Patrick ni mtoto wake, tena hakupewa taarifa kama mtoto wake anaumwa. Alikuwa anasoma kwenye Instagram tu. Akipiga simu hakuna kinachoendelea na wala hapokelewi.

Mambo haya ya kuvutana yaliendelea hadi mtoto alipofariki ndipo Peter sasa alipojitokeza na kusema yeye ndiye baba halali wa mtoto Patrick na ana vyeti vyote. Wakati Patrick anazaliwa, mamake, Bi. Rose alikuwa mke halali wa Peter Komu. Kwa mfumo wa maisha ya kawaida, kitanda hakizai haramu na huwezi kuzaa na mke wa mtu. Hali halisi Casto alikosea na ndio maana hata hakuonekana kuvutana na suala zima la nani baba halali wa mtoto.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]