Mtumiaji:Mtongori
Matinde John | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Mtongori |
Alizaliwa | 28-Feb-1992 |
Nchi | Tanzania |
Kazi yake | Mhandisi(Huawei
Tigo HQ) |
Ndoa | Rose charles Maryoba |
Wazazi | John Marwa na Bhoke Magabe |
Karibu kwenye ukurasa wa Matinde John, ni mhariri wa Wikipedia ya Kiswahili na Kiingereza kutoka nchini Tanzania.Pia Matinde John alimaliza shahada ya kwanza ya Uhandisi wa Electrokia na Mawasiliano 2018 kutoka chuo kikuu cha Mtakatifu Yosefu kilichopo Mbezi Dar es salaam Tanzania .Kwa sasa yupo Huawei Tigo makao makuu Dar es salaam
Kuzaliwa
[hariri | hariri chanzo]Matinde John alizaliwa tarehe (28 feb 1992 ) wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani .Pia Matinde John ni mtoto wa nne kwenye familia ya John Marwa Masero (Chegere) iliyopo Kijiji cha Nyang'aranga kata ya Mugeta mkoa wa Mara, Majina mengine anaitwa Matinde John, Mtongori ndo jina maarufu hapo Kijijini kwao Nyang'aranga
Shule ya Msingi
[hariri | hariri chanzo]Matinde John alisoma shule ya msingi Nyang'aranga iliyopo Wilaya ya Bunda Mara toka darasa la kwanza mpaka darasa la tano na baadae kuhamia shule ya Msingi Kiluvya wilaya ya Ubungo iliyopo mkoa wa Dar es salaam.Baada ya kumaliza darasa la saba alifaulu na kuchaguliwa shule ya sekondari ya kibamba. [1]
Shule ya Sekondari
[hariri | hariri chanzo]Matinde John alianza shule ya Kibamba sekondari toka mwaka (2008-2011) kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha nne masomo ya Sayansi .Alifaulu kidato cha nne.[2] mwaka 2011 na kuchagulia kidato cha tano Azania[3] .Mwaka wao ndo walikuwa wa pili kumaliza kidato cha nne baada ya kuanzishwa Kibamba.Kibamba sekondari ni mojawapo ya shule za kata katika kata ya Kibamba wilaya mpya ya Ubungo mkoa wa Dar es salaam[4].Ubungo ni mojawapo ya wilaya mpya zilizoongeza Tanzania Ubungo imeongezeka baada ya wilaya ya Kinondoni kugawanyika na kupatika wilaya ya kinondoni na Ubungo
Shule ya kidato cha tano na sita
[hariri | hariri chanzo]Pia Matinde John alisoma Azania[5] sekondari PCM.(Physics chemistry na Mathematics) toka mwaka 2012-2014
Chuo Kikuu
[hariri | hariri chanzo]Alisoma chuo kikuu cha Mtakatifu Yosefu (St Joseph college of Engineering and Technology) kilichopo Mbezi Dar es salaam Tanzania toka mwaka (2014-2018).Mtongori ni mhandisi wa Electrokia Na Mawasiliano inayojulikana kama (Bachelor of Engineering in Electronics and Communication Engineering)
Maisha yake
[hariri | hariri chanzo]Matinde John kwa sasa amemaliza shahada yake ya kwanza katika chuo kikuu cha Uhandisi kilichopo wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es salaam Mtongori anafanya kazi ya Uhandisi wa Mawasiliano Huawei Tanzania-Tigo Makao makuu (PSSF TOWER)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.sitelinks.info/search/matokeo-ya-darasa-la-saba-2007/
- ↑ http://196.44.162.33/necta2011/CSEE%202011/s3091.htm
- ↑ https://www.scribd.com/doc/51144533/Orodha-Ya-Wavulana-waliochaguliwa-kujiunga-na-kidato-cha-tano-2011
- ↑ http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Dar-yapendekeza-wilaya-mbili-mpya/1597296-2291018-11ugp8bz/index.html
- ↑ http://www.azaniasecondary.sc.tz/