Mtumiaji:Lucas559/Mimba ya ectopic
Lucas559/Mimba ya ectopic | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Madaktari wa uzazi na Madaktari wa mfumo wa uzazi wa mwanamke |
Dalili | Maumivu ya tumbo, kuvuja damu ukeni[1] |
Sababu za hatari | Ugonjwa wa kuvimba kwenye fupanyongo, uvutaji wa tumbaku, upasuaji wa awali wa mirija ya uzazi, historia ya utasa, matumizi ya teknolojia ya kutoa usaidizi wa uzazi[2] |
Njia ya kuitambua hali hii | Vipimo vya damu vya human chorionic gonadotropin (hCG), vipimo vya picha vinavyotumia mawimbi ya sauti (ultrasound)[1] |
Utambuzi tofauti | Mimba kuharibika, kujipinda kwa ovari, kufura ghafla kwa kidole tumbo[1] |
Matibabu | Methotrexate, upasuaji[2] |
Utabiri wa kutokea kwake | Vifo vya 0.2% (nchi zilizoendelea), 2% (nchi zinazoendelea)[3] |
Idadi ya utokeaji wake | ~1.5% ya mimba (nchi zilizoendelea)[4] |
Mimba inayomea nje ya uterasi (Ectopic pregnancy) ni tatizo la ujauzito ambapo kiinitete hujishikilia nje ya uterasi.[4] Ishara na dalili kimsingi ni pamoja na maumivu ya tumbo na kutokwa na damu ukeni, lakini chini ya asilimia 50 ya wanawake walioathirika wana dalili hizi zote.[1] Maumivu hayo yanaweza kuelezewa kuwa mkali, hafifu au yanayokuja na kutoweka.[1] Maumivu yanaweza pia kuenea hadi kwa bega ikiwa uvujaji wa damu ndani ya tumbo.[1] Kuvuja damu nyingi kunaweza kusababisha mapigo ya moyo ya haraka, kuzirai au mshtuko.[4][1] Isipokuwa kwa nadra sana fetasi haiweza kukua katika hali hiyo.[5]
Vihatarishi vya mimba inayomea nje ya uterasi ni pamoja na ugonjwa wa kuvimba kwenye fupanyongo, mara nyingi kutokana na maambukizo ya klamidia; uvutaji wa tumbaku; upasuaji wa awali wa mirija ya uzazi; historia ya utasa; na matumizi ya teknolojia ya usaidizi wa uzazi.[2] Wale ambao hapo awali walikuwa na mimba inayomea nje ya uterasi wako katika hatari kubwa zaidi ya kuathirika tena.[2] Mimba nyingi zinazomea nje ya uterasi (90%) hufanyika kwenye mirija ya uzazi, ambayo hujulikana kama mimba inayomea kwenye mirija ya uzazi,[2] lakini upandikizaji unaweza pia kutokea kwenye seviksi, ovari au ndani ya tumbo.[1] Utambuzi wa mimba inayomea nje ya uterasi kwa kawaida hufanywa kwa vipimo vya damu vya homoni ya gonadotropini ya chorioniki ya binadamu (human chorionic gonadotropin, hCG) na vipimo vya picha vinavyotumia mawimbi ya sauti.[1] Hii huenda ikahitaji vipimo vya zaidi ya mara moja.[1] Vipimo vya picha vinavyotumia mawimbi ya sauti hufanya kazi vizuri zaidi vinapofanywa ndani ya uke.[1] Visababishi viingine vya dalili zinazofanana ni pamoja na: kuharibika kwa mimba, ovari kujipinda kwa ovari na kufura ghafla kwa kidole tumbo.[1]
Kinga ya mimba inayomea nje ya uterusi inafanywa kwa kupunguza vihatarishi kama vile maambukizo ya klamidia kupitia uchunguzi na matibabu.[6] Ingawa baadhi ya mimba zinazomea nje ya uterasi zinaweza kutatuliwa bila matibabu, mbinu hii haijafanyiwa utafiti vizuri kufikia mwaka wa 2014.[2] Matumizi ya dawa ya methotrexate hufanya kazi pamoja na upasuaji katika baadhi ya matukio.[2] Hasa, inafanya kazi vizuri wakati kiwango cha beta-HCG ni kidogo na ukubwa wa mimba hiyo ni ndogo [2] Upasuaji bado unapendekezwa ikiwa mrija umepasuka, kuna mpigo wa moyo wa fetasi au hali ya afya ya mtu siyo imara.[2] Upasuaji unaweza kuwa wa laparoskopi au kupitia chale kubwa zaidi, inayojulikana kama laparotomi . [4] Matokeo kwa ujumla ni bora kwa wanawake wanaopata matibabu.[2]
Kiwango cha watoto wanaozaliwa hai katika mimba inayomea nje ya uterasi ni takriban asilimia 1% na 2% katika nchi zilizoendelea, ingawa kinaweza kufikia hadi asilimia 4% kwa wale wanaotumia teknolojia ya kutoa usaidizi wa uzazi.[4] Ndiyo kisababishi kikuu cha vifo miongoni mwa wanawake katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito ikiwa ni takribani asilimia 10% ya vifo vyote.[2] Katika nchi zilizoendelea matokeo yameboreka huku katika nchi zinazoendelea mara nyingi matokeo yamesalia kuwa mabaya.[6] Hatari ya vifo miongoni mwa wamama walio katika nchi zilizoendelea ni kati ya asilimia 0.1 na 0.3 huku katika nchi zinazoendelea ikiwa ni kati ya asilimia moja hadi tatu.[3] Maelezo ya kwanza yanayojulikana ya mimba inayomea nje ya uterasi ni ya Al-Zahrawi katika karne ya 11.[6] Neno "ectopic" linamaanisha "nje ya mahali panapofaa".[7]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.00 1.01 1.02 1.03 1.04 1.05 1.06 1.07 1.08 1.09 1.10 1.11 Crochet JR, Bastian LA, Chireau MV (2013). "Does this woman have an ectopic pregnancy?: the rational clinical examination systematic review". JAMA. 309 (16): 1722–9. doi:10.1001/jama.2013.3914. PMID 23613077.
- ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 Cecchino GN, Araujo Júnior E, Elito Júnior J (Septemba 2014). "Methotrexate for ectopic pregnancy: when and how". Archives of Gynecology and Obstetrics. 290 (3): 417–23. doi:10.1007/s00404-014-3266-9. PMID 24791968.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 Mignini L (26 Septemba 2007). "Interventions for tubal ectopic pregnancy". who.int. The WHO Reproductive Health Library. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2 Aprili 2015. Iliwekwa mnamo 12 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 Kirk E, Bottomley C, Bourne T (2014). "Diagnosing ectopic pregnancy and current concepts in the management of pregnancy of unknown location". Human Reproduction Update. 20 (2): 250–61. doi:10.1093/humupd/dmt047. PMID 24101604.
- ↑ Zhang J, Li F, Sheng Q (2008). "Full-term abdominal pregnancy: a case report and review of the literature". Gynecologic and Obstetric Investigation. 65 (2): 139–41. doi:10.1159/000110015. PMID 17957101.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 Nama V, Manyonda I (Aprili 2009). "Tubal ectopic pregnancy: diagnosis and management". Archives of Gynecology and Obstetrics. 279 (4): 443–53. doi:10.1007/s00404-008-0731-3. PMID 18665380.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Cornog, Mary Wood (1998). Merriam-Webster's vocabulary uilder. Springfield, Mass.: Merriam-Webster. uk. 313. ISBN 9780877799108. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-10.