Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Idd Mwimbe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Idd Mohamed Mwimbe alizaliwa tarehe 29/08/1988 katika kijiji cha Mapinga wilayani Bagamoyo [1] mkoa wa Pwani.Ni mtoto wa kwanza katika familia ya Mzee Mohamed Mwimbe ya Bagamoyo.

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi Majengo iliyopo wilayani Bagamoyo na kumaliza mwaka 2003. Kisha alijiunga na elimu ya upili katika shule ya Sekondari Kiwangwa mwaka mmoja baadae alihamia na kumaliza katika shule ya Bagamoyo Sekondari iliyopo Bagamoyo. Baadae alichaguliwa kujiunga na kidato cha 5 katika Shule ya Sekondari ya wavulana Kwiro iliyopo wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro . Alisoma kwa miezi kadhaa kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Ununio iliyopo Dar Es Salaam ambapo alimalizia kidato cha sita. Mwaka 2012 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo alichukua Shahada ya Sanaa na Elimu na kumaliza mwaka 2015.

VITABU ALIVYOWAHI ANDIKA

[hariri | hariri chanzo]

Idd Mwimbe ni mtunzi na mwandishi wa fasihi ya kiswahili kwani hadi sasa amefanikiwa kuchapisha vitabu vifuatavyo:

Kitabu cha Msitu Mweusi ameshirikiana na mwandishi mwingine aitwaye Happy Mademla

MISWAADA AMBAYO HAIJATOKA

[hariri | hariri chanzo]

Hadi sasa ana miswada kadhaa ambayo bado haijatoka ikiwemo:

TUNZO ALIZOTUNUKIWA

[hariri | hariri chanzo]

Idd Mwimbe alichaguliwa kuwa mshairi bora Tanzania2015/2016 katika Tunzo ya Profesa Ebrahim Hussein inayoendeshwa na Tanzania Gatsby Trust . Pia mwaka 2017 alichaguliwa kuwa katibu Mkuu Taifa wa Umoja wa Washairi Tanzania (UWASHATA) ambapo cheo hiko anakitumikia hadi sasa. Idd Mwimbe pia ni muasisi wa Jukwaa la mtandaoni la washairi linaloitwa MAJAGINA WA USHAIRI ambalo linajumuisha washairi mbalimbali kutoka nchi kadhaa za Afrika na Ulaya pia. Mbali na ushairi pia Idd Mwimbe ni mshauri na mhamasishaji katika mambo mbalimbali kuhusu kiswahili . Kwasasa anaishi Bagamoyo.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Idd Mwimbe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. https://www.dw.com/sw/kutana-na-mshairi-chipukizi-kutoka-pwani-ya-tanzania/av-43066953
  2. https://www.worldcat.org/title/hekalu-limechafuka/oclc/1003489189