Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Erick J. Budeba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

MAKALA YA KWANZA

[hariri | hariri chanzo]

Saskia Luutsche Ozinga (alizaliwa 1960 huko Beverwijk) [1] ni mwanaharakati wa mazingira kutoka nchini Uholanzi. Saskia ni mwezeshaji wa Forest Movement Europe (FME) na mwanzilishi mwenza wa shirika lisilo la kiserikali la FERN. Alikuwa mratibu wa kampeni ya Forest Movement Europe (FME), mnamo mwaka 1995 mpaka 2017. [2]

Saskia Ozinga ana shahada ya uzamili katika Biolojia kutoka Chuo Kikuu cha Wageningen na shahada ya uzamili katika Huduma ya Afya kutoka Chuo Kikuu cha Utrecht, Uholanzi. Baada ya kufanya kazi kama mwalimu wa sayansi ya mazingira katika Chuo Kikuu cha Utrecht, Saskia Ozinga alijiunga na taasisi ya Friends of the Earth. Alifanya kazi kama afisa elimu wa taasisi ya Friends of the Earth nchini Uholanzi kuanzia 1987 hadi 1990, alipochukua nafasi ya mwanaharakati wa misitu. Mnamo 1991, Saskia alichukua jukumu la mwezeshaji wa Jumuia mpya ya Forest Movement Europe (FME), jukumu ambalo bado anashikilia hadi sasa.

Mnamo Machi 1995 Saskia pamoja na Sian Pettman walianzisha, shirika la FERN likiwa na mamlaka ya kufuatilia shughuli za Umoja wa Nchi za Ulaya kuhusiana na misitu. Saskia Ozinga pia ni mwanachama wa bodi ya Forest Peoples Programme, Stichting Tropenbos International na Taiga Rescue Network, na mjumbe wa kamati ya uongozi ya World Rainforest Movement.

Saskia Ozinga aliolewa na Mark Gregory na kupata mtoto wa kike huko Oxfordshire. Mark ni mwandishi wa habari wa zamani wa BBC Radio World Service.

  1. Small bio (page 14)
  2. FERN site - [1]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Erick J. Budeba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


MAKALA YA PILI

[hariri | hariri chanzo]

Enriqueta Medellín (10 Desemba 1948 - 6 Januari 2022) alikuwa daktari wa upasuaji wa Mexiko na mwanamazingira alielelewa katika Jiji la Mexiko. Tangu akiwa mdogo alishiriki katika miradi ya kusafisha jiji na akapendezwa kujishughulisha na masuala ya magonjwa na mazingira. Alipata shahada kama daktari wa upasuaji kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Autonomous cha Mexiko na alibobea katika elimu ya vinasaba vya binadamu. Pia alisomea elimu ya mazingira na usimamizi.

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

María Enriqueta Medellín Legorreta alizaliwa tarehe 10 Desemba 1948 katika Jiji la Mexico. Mama yake alifahamika kwa jina la Enriqueta Legorreta López na baba yake Mario Medellín Ocádiz. Kwa imani yake ya kikatoliki alibatizwa siku mbili baada ya kuzaliwa kwake katika Kanisa Katoliki la Parokia ya San Cosme.[1][2][3] Alikuwa na kaka mkubwa aitwaye Mario, ambaye ni mwanamuziki, na wadogo zake watatu, Alejandro Claudio, Juan, pamoja na Rodrigo. Baba yake alikuwa mhasibu na mwanzilishi wa kiwanda cha icecream, huku mama yake akiwa mwimbaji na mwanaharakati. Legorreta pia alijitolea katika Chama cha Ikolojia cha Coyoacán kijulikanacho kama Asociación Ecológica de Coyoacán na kuwashirikisha watoto wake katika shughuli za kusafisha Bustani ya Kifalme ya San Lucas, Parque Real de San Lucas iliopo mjini Coyoacán.[4] Kifo cha mdogo wake aitwaye Juan mnamo mwaka 1969 kutokana na saratani kilichochea udadisi wa Medellín kuhusu uhusiano kati ya ugonjwa na mazingira.[3][5]

  1. Baptismal Registry 1948, p. 357.
  2. Rodríguez 2022.
  3. 3.0 3.1 Sociedad de Autores y Compositores de México 2019.
  4. Cano Sotomayor & Ramírez Camino 2014, p. 148.
  5. Muñoz 2013.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Erick J. Budeba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.