Mto Muni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mto Muni

Muni ( Kifaransa : Rivière Muni, Kihispania: Río Muni ) ni mdomo wa mito mbalimbali inayoungana kabla ya kuishia kwenye Bahari Atlantiki. Muni inaunganisha mito kadhaa ya Guinea ya Ikweta na Gabon . [1] [2] Sehemu ya urefu wake ni sehemu ya mpaka na Gabon . Ni kutoka kwenye mdomo huo ambako jina la Río Muni lilichukuliwa, ambayo ni sehemu ya bara ya Guinea ya Ikweta.

Mito[hariri | hariri chanzo]

Muni inalishwa upande wa kaskazini na mto Congue na Mto Mandyani na kutoka mashariki na Mitong, Mven na Mto Timboni.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Equatorial Guinea.
  2. A directory of African wetlands By R. H. Hughes, J. S. Hughes, p. 501 (on Google Books: )