Msaada:Jaribio
Ukurasa wa jaribio ni ukurasa ambako una kila uhuru kufanya majaribio ya fomati na maudhui.
1. Sandbox / Sanduku la mchanga
Ukurasa wa Wikipedia:Sanduku la mchanga unafaa kwa majaribio madogo: humo unaweza kubadilisha chochote kilichopo ila hakitadumu.
2. Jaribio katika nafasi yako ya mtumiaji
Kama umejiandikisha katika wikipedia ya Kiswahili, umeunda nafasi yako ya pekee. Umeshapata ukurasa wa "Mtumiaji:JINA". (Ukibofya hapa ukurasa wako wa mtumiaji unafunguliwa, lakini utaupata pia ukibofya jina lako juu kwenye ukurasa huu.)
Usipofanya kitu kingine baada ya kujiandikisha, umeshapata ukurasa wako (unapoweza kujitambulisha ukipenda) na ukurasa wako wa majadiliano, ambako watumaji wengine wanaweza kukuandikia ujumbe.
Ukurasa wako unakupa nafasi ya kuunda kurasa ndogo (subpages). Kama ukurasa wako unaitwa "Mtumiaji:JINA", unaweza kuongeza neno au namba nyuma yake. Kwa mfano ukibofya "Mtumiaji:JINA/Jaribio1" unaunda ukurasa ndogo ya ziada "Jaribio1" katika nafasi yako! Hakuna kikomo, unaweza kuunda kurasa nyingi za aina hii. Katika nafasi yako usiweke jamii bado wala interwiki.
Kwenye kurasa hizo za ziada ndani ya nafasi yako ya mtumiaji unaweza kuanzisha makala. Usipomaliza, hifadhi tu, endelea kesho. Unaweza kuanza kutafsiri na kuendelea siku nyingine. Unaweza kumpa rafiki URL ya ukurasa huo na kumwomba apitilie au asahihishe. Rafiki yako anaweza kutumia Msaada:Checklist akikagua makala yako.
3. Kuhamisha maudhui kuwa makala kamili
Ukiridhika unaanzisha ukurasa kwenye nafasi kuu (article namespace) na kuunda makala rasmi.
Una njia mbili: A. Kwanza fungua ukurasa wako wa majaribio, bofya "hariri chanzo", kopi yote. Anzisha makala mpya kwa kuandika lemma mpya (yaani jina la makala mpya) katika dirisha la "Kutafuta", bofya enter. Utaona mstari "Anzisha ukurasa wa "JINA" katika wiki hii!Tazama pia matokeo kupatikana." "Jina" inaonekana kwa rangi nyekundu. Bofya hapa na ukurasa mpya unafunguliwa. Sasa mwaga humo matini uliyoandaa. Hifadhi umeshaunda makala mpya.
B. Kwenye ukurasa wako wa majaribio, 1) bofya "Zaidi" kwenye menyu ya juu. 2) Chagua "Hamisha". Katika ukurasa angalia chini ya 3) "Kichwa cha habari kipya:" - hapa bofya pembetatu ndogo , 4) badilisha "Mtumiaji" iwe "(Kuu)". 5) Halafu uandike jina la makala mpya upande wa kulia. 6) Hatimaye bofya chini "Hamisha Ukurasa".
4. Faida ya kuanza kwenye nafasi ya mtumiaji:
Faida ni: ukianzisha makala yenye makosa mengi, inaweza kupelekwa haraka kwenye ukurasa wa "Wikipedia:Makala kwa ufutaji". Hapa katika nafasi yako hakuna atakayekusumbua (isipokuwa ukiitumia vibaya kwa matangazo ya kibiashara au matusi!) una nafasi ya kunyosha kila kitu hadi umeridhika.
Ni faida kubwa hasa kwa wanawikipedia wapya, lakini pia kwa wengine wanaoanza kazi kubwa isiyomalizika mara moja.
5. Msaada wa Ukaguzi
Unaweza kutumia Msaada:Checklist ukipitilia makala yako au ya mtu mwingine.