Mr. Blue

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mr Blue)
Mr. Blue
Mr. Blue kwenye pozi.
Mr. Blue kwenye pozi.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Kheri Sameer Rajabu
Amezaliwa 14 Aprili 1987 (1987-04-14) (umri 36)
Aina ya muziki R&B na Bongo Flava
Kazi yake Mwimbaji
Ala Sauti
Miaka ya kazi 1999-
Studio G. Records, Dhahabu Records, 41 Records
Ame/Wameshirikiana na TID
Lady Jay Dee, K-Lyin

Khery Sameer Rajab (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Mr. Blue; amezaliwa 14 Aprili 1987) ni msanii wa muziki wa R&B na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania.

Alifanikiwa kujizolea umaarufu mkubwa huku akipendwa na wapenzi na mashabiki, mara tu baada ya kuingia katika fani ya muziki na wimbo wake 'Mr Blue'. Ambapo baadaye ikaja kuwa kama ndiyo jina lake la kisanii.

Mr Blue alikuwa gumzo na wimbo 'Mr Blue' kabla ya kuja kupata umaarufu zaidi na wimbo wake wa 'Mapozi', ambao ndiyo uliomzidishia kupendwa kutokana na mpangilio wa mashairi na sauti aliyotumia pamoja na maujanja ya ala ya muziki wenyewe.

Maisha ya awali

Mr Blue alizaliwa 14 Aprili mwaka 1987, ni mtoto wa tatu kati ya wanne kwa kuzaliwa katika familia ya mzee Sameer Alhaji Alhad Ally mwenye asili ya Ki-Sudan.

Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya Gerezani ambako alihitimu mwaka 1999, lakini hakuweza kumaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam, ambako aliishia kidato cha pili mwaka 2004.

Alipoulizwa ni kitu gani kilichosababisha hadi kukatisha masomo ya sekondari, alisema: "Muziki ndio ulionifanya nikaacha shule, lakini bado nahitaji kusoma na baada ya muda kadhaa nategemea kujiendeleza kimasomo nje ya nchi." Japo baadae mwaka 2014 alikuja kufafanua changamoto zilizokuwa zikimkabili katika kipindi cha televisheni kiitwacho mkasi, kinachoongozwa na Salama Jabir, kikubwa alisema mahitaji ya kifedha yalikuwa makubwa na ulifika wakati alilazimika aidha kuchagua muziki au shule, kwa kuwa muziki ulikuwa ukitatua tatizo la kifedha, basi hakuwa na budi kuchagua muziki

Akizungumzia hatua waliyochukua wazazi wake kutokana na kuacha kwake shule kwa sababu ya muziki, anasema hawakumgombeza kwani walijua ni ujana tu unamsumbua huku wakiamini itafikia wakati atatulia

Muziki

Mr Blue alianza kujihusisha na masuala ya muziki mwaka 1999, na kilicho sababisha ajiingize katika fani hiyo ni kaka zake waaliojulikana kwa majina ya The Boy Stain na Obrey, ambao nao walikuwa wakijihusisha na suala zima la muziki.

Lakini hakuanza kuimba moja kwa moja, bali alikuwa akifuatilia tu jinsi gani muziki unavyokua, na mwaka 2001 ndipo nilipojiingiza zaidi kwa kuanza kuimba katika sherehe mbalimbali za 'Macamp.

"Mwaka 2003 kuelekea 2004 ndipo alipotoka na wimbo wake wa 'Mr Blue' ambao ndiyo ulioanza kumapatia umaarufu.

Wakati akitamba na kibao chake hicho, lakini hakutaka mashabiki wamsahau mapema, hivyo aliamua kutoa kibao kingine kilichokwenda kwa jina la 'Mapozi', ambacho kilimtangaza na kupiga hatua kupitia nyimbo hizo.

Mr Blue ambaye albamu yake ya kwanza ilikwenda kwa jina la 'Mr Blue' na ya pili ni 'Yote Kheri'.

Pia anawashukuru mama yake mzazi Halima Rajab na baba yake Sameer Alhaj Alhad Ally kwa kumruhusu kujikita katika muziki.[1] Pia aliwahi kuwa na mahusiano na msanii mwenzake anayejulikana kama Naj anayeishi jijini London. uhusiano huo uliisha kitambo kidogo na sasa Mr. Blue ana mke na sasa hivi anatamba nyimbo aliyoshilikishwa na msanii mwenzake ambaye anajulikana kama shetta nyimbo ambayo wamefanyakazi watu watatu ambao ni shetta mr blue na jux

Marejeo

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mr. Blue kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.