Mpango wa Feed the Future
Mpango wa Feed the Future (FTF) ulizinduliwa mwaka 2010 na serikali ya Marekani wakati wa utawala wa Barack Obama ili kukabiliana na njaa duniani na ukosefu wa usalama wa chakula. Kulingana na Feed the Future, huo ni "mpango wa serikali ya Marekani wa kukabiliana na njaa na usalama wa chakula duniani.[1]
Mpango wa Feed the Future ulianza kama jitihada "ya kukabiliana na ongezeko la bei za chakula duniani mwaka 2007 na 2008." Mwaka 2009, Rais Barack Obama aliahidi dola bilioni 3.5 kwa kipindi cha miaka mitatu kwa mpango wa kimataifa wenye lengo la kukabiliana na njaa na umasikini; mnamo Mei 2010, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilizindua Mpango wa Feed the Future. Mpango huu ulitengenezwa na Wizara ya Mambo ya Nje na unaratibiwa hasa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). [2] Malengo makuu ya mpango huo ni kuendeleza maendeleo ya kilimo duniani, kuongezeka kwa uzalishaji wa chakula na usalama wa chakula, na kuboresha lishe hasa kwa watu walio katika mazingira magumu kama vile wanawake na watoto. [2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Feed the Future". Iliwekwa mnamo 2023-10-16.
- ↑ 2.0 2.1 "About | Feed the Future". Feedthefuture.gov. Iliwekwa mnamo 2013-11-25.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |