Mnara wa taa wa Don Luis
Mnara wa taa wa Don Luis au Mnara wa taa wa Ilhéu dos Pássaros ni mnara wa taa uliopo juu ya kisiwa cha Ilhéu dos Pássaros, karibu na kisiwa cha São Vicente (Cape Verde) | São Vicente katika vifungu vya visiwa vya Barlavento, nchini Cape Verde.
Mnara huu wa taa unamilikiwa na kusimamiwa na Mkurugenzi wa Bandari na Bahari.[1].
Historia
[hariri | hariri chanzo]Ilhéu dos Pássaros ni eneo linalotenganisha ghuba ya Porto Grande na mkondo wa São Vicente. Kisiwa hiki kinapatikana magharibi mwa Ponta João Ribeiro kisiwa kikuu ni São Vicente kaskazini magharibi mwa Cape Verde; kilometa 3.5 kaskazini magharibi mwa bandari ya Mindelo. Mnara huu wa taa upo eneo la juu kabisa la kisiwa hicho, majengo ya kimkakati yapo takribani nusu umbali. Mnara huu unaweza kufikiwa kwa njia ya majini pekee kwa kufuata mfereji mwembamba kwa kutumia mtumbwi mashariki mwa bandari ya Mont Cara.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Mnara huu ulijengwa mwaka 1882, wakati wa kuongoza vyombo vya majini kuingia na kutoka katika ghuba ya Porto Grande, pia wakati wa kutia nanga bandari ya Mindelo. Kwa sasa, inaongoza meli zinazosimama na kuondoka kutoka ghuba ya Porto Grande, eneo la ndani lenye usafiri wa boti na meli zinazoingia na kutoka. Mnara huu wa taa ulipewa jina baada ya mfalme wa Ureno Louis I (Don Luis) ambaye alikua ndiye mfalme wa mwisho wa Ureno. Mnara huu wa Taa ni mweupe wenye pande sita wenye umbo la piramidi ikiwa na tochi ya rangi nyekundu yenye ukubwa wa mita 5. Inawaka katika urefu wa takribani mita 86, kwa kutoa mwanga mweupe mara tatu kila baada ya sekunde 12. Umbali wa mwanga huu ni takribani kilomita 26.
Sifa
[hariri | hariri chanzo]Kujirudia ndani ya sekinde 12: (W-W-W)
- Mwanga: Sekunde 1
- Giza: Sekunde 2
- Mwanga: Sekunde 1
- Giza: Sekunde 2
- Mwanga: Sekunde 1
- Giza: Sekunde 5
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Mnara wa taa wa Don Luis
-
Mnara wa taa wa Don Luis mwaka 2008
-
Ilheu dos Passaros Santo Antao
-
Ramani ya Bela-vista-net-Sao Vicente