Mkoa wa Maritime, Togo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkoa wa Maritime (Pwani) nchini Togo

Mkoa wa Maritime[1] ndio mkoa wa kusini kabisa kati ya mikoa mitano ya Togo. Iko kwenye ufuo wa bahari ya Atlantiki ikitazama Hori ya Benin. Jina "Maritime" linamaanisha "bahari" au kwa lugha nyingine ni mkoa wa pwani.

Makao makuu ya mkoa yako mjini Lome ambayo ni pia mji mkuu wa kitaifa. Mkoa huo ni mkoa mdogo zaidi kieneo una idadi kubwa ya watu.

Miji mingine mikubwa katika mkoa wa Maritime ni pamoja na Tsevie na Aneho .

Mkoa wa Kati umegawanywa katika wilaya za Ave, Bas-Mono, Golfe, Lacs, Vo, Yoto, na Zio . [2]

Mkoa wa Kati uko kusini mwa Mkoa wa Plateaux. Upande wa magharibi, unapakana na Ghana, na upande wa mashariki iko Benin.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Tamka ma-ri-tim, herufi ya "e" mwishoni ni kimya
  2. "Annuaire Statistique du Togo (2010-2013)" (kwa Kifaransa). October 2019. Iliwekwa mnamo 2021-08-06.  Check date values in: |date= (help)