Mke Wangu Tuelewane

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Mke Wangu Tuelewane"
Wimbo wa Msondo Ngoma
Umetolewa 1999-2000
Umerekodiwa 1999-2000
Aina ya wimbo Muziki wa dansi
Lugha Kiswahili
Urefu 8:21

Mke Wangu Tuelewane ni jina la kutaja wimbo uliotungwa na kuimbwa na kundi zima la Msondo Ngoma kati ya miaka ya tisini na elfu mbili mwanzoni. Moja kati ya nyimbo zilizotamba sana katika miaka hiyo. Mashairi yake anazungumzia maelewano baina ya mume na mke. Mke anatia kisirani katika masuala mbalimbali - nongwa mwanzo mwisho. Mke anasihiwa ya kwamba "hata majembe wakati fulani hugongana, sembuse mimi na wewe" maneno ya Maalim Gurumo. Ndani yake, kuna waimbaji kama vile Hassan Bichuka ambaye ameonekana kushika sehemu kubwa ya wimbo huu.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]