Nenda kwa yaliyomo

Mimba ya fumbatio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mimba ya fumbatio
mimba nje ya mfuko wa uzazi
Abdominal pregnancy
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuObstetrics Edit this on Wikidata
ICD-10O00.0.O83.3.
ICD-9633.00

Mimba ya fumbatio ni aina ya mimba ya nje ya mji wa mtoto ambapo mimba inapachikwa ndani ya kifuko cha ngozi ya fumbatio nje ya neri ya falopu au ovari na si katika kano pana shikilizi.[1] Ingawa nadra, mimba za fumbatio huwa na kiwango cha juu zaidi cha vifo kuliko mimba ya nje ya neri ya falopu kijumla,lakini, katika matukio fulani, huweza kuzaliwa watoto hai.

Takriban asilimia 1 ya mimba ya nje ya mji wa mtoto nchini Marekani ni ya fumbatio, au 10 kati ya kila mimba 100,000.[1] Ripoti kutoka Nigeria yaonesha kuwa matukio katika nchi hiyo ni 34 katika kila uzazi 100,000.[2] Sababu za hatari ni sawa na za mimba ya neli huku magonjwa ya zinaa yakiwa ndiyo yanayoleta athari kubwa.[3] Kiwango cha vifo vya wajawazito kinakadiriwa kuwa juu ya 5 kwa kila kesi 1,000, ikiwa takribani mara saba kijumla juu mimba ya nje wa mji wa mtoto, na mara 90 juu ya kiwango cha uzaaji (takwimu za Marekani).[1]

Anatomia

[hariri | hariri chanzo]

Maeneo ya upachikaji ni pamoja na utando wa nje ya mji wa mimba, kifuko cha mji wa mimba (kuldesaki ya Douglas), omentamu, matumbo na utando wa fumbatio, mezosalfiniksi, na utando wa ukuta wa fupanyongo na ukuta wa fumbatio.[1][4]. Mji wa mtoto unaokua unaweza kushikiliwa katika viungo kadhaa ikiwa ni pamoja na neri na ovari. Maeneo mengine nadra huwa ini na wengu.[5] hivyo kusababisha mimba ya ini [6] au mimba ya wengu, katika usanjari huo.[7] Hata mimba ndogo ya kitangaa imepatikana katika mgonjwa ambapo mimba ulikuwa ukikua upande wa chini wa kitangaa.[8]

Ulinganisho wa upachikaji wa msingi na wa upili

[hariri | hariri chanzo]

Mimba ya fumbatio ya msingi inamaanisha mimba iliyopachikwa moja kwa moja katika mwina wa fumbatio na viungo vyake, isipokuwa katika neli na ovari, mimba kama hiyo ni nadra sana, visa 24 tu ndivyo vimeripotiwa tangu 2007.[9] Kwa kawaida mimba ya fumbatio ni ya upili ikiwa upachikaji umetokana na upachikaji katika neli (mara chache kutoka katika ovari) na kupachikwa tena.[4] Ili kuagua mimba nadra ya fumbatio ya msingi, vigezo vya Studdiford vinafaa kutimika: neli na ovari lazima ziwe katika hali ya kawaida, isiwe na miunganisho isiyo ya kawaida (nasuri) kati ya chupa ya uzazi na mwina fumbatio, na kwamba mimba ihusiane na utando wa fumbatio pekee bila ishara kwamba kulikuwa na mimba ya neli kwanza.[5]

Mgonjwa mwenye mimba ya fumbatio anaweza tu kuonyesha dalili za kawaida ya mimba au dalili zisizo maalum kama vile maumivu ya tumbo, kutokwa na damu ukeni, na / au dalili za maumivu ya utumbo.[4] Mara nyingi uaguzi wa mimba ya fumbatio hukosewa.[2] Hata hivyo, ni hali hatari inayoweza kutokwa damu ndani ya mwili na kusababisha dharura ya kimatibabu na kwa mshtuko wa upungufu wa damu na inaweza kuua, sababu nyingine za vifo vya wazazi walio na mimba ya fumbatio ni pamoja na toksemia, anemia, mvilio wa damu mapafuni, tatizo la kuganda damu, na maambukizi.[3]

Shaka ya kuwepo kwa mimba ya fumbatio huibuka wakati sehemu za mtoto zinaweza kuhisika kirahisi, au mkao si wa kawaida. Sonografia ni muhimu sana katika uaguzi kwa kuwa inaweza kuonyesha kuwa mimba iko nje ya uterasi tupu, hakuna uoevu wa amioni kati ya kondo na kijusi, hakuna ukuta wa mji wa mtoto unaozunguka kijusi, sehemu za kijusi ziko karibu na ukuta wa fumbatio, na kijusi kimelele vibaya.[3] MRI pia imetumika kwa mafanikio kuagua mimba ya fumbatio.[9] Ongezeko la viwango vya protini ya alfa pia ni kidokezo kingine cha kuwepo mimba ya fumbatio.[10]

Matibabu

[hariri | hariri chanzo]

Matibabu yanayoweza kutolewa ni pamoja na upasuaji unahusisha kuondolewa kwa mimba kutumia laparoskopi au laparotomi, matumizi ya methotreksate, uwekaji vidonge, na mchanganyiko wa haya. Uchaguzi wa mbinu kwa ukubwa huamuliwa na hali ya mimba hiyo. Kwa ujumla, matibabu inadhihirishwa wakati uaguzi unapofanyika, hata hivyo, hali ya mimba ya fumbatio iliyokaa huwa ngumu zaidi.

Mimba ya fumbatio iliyoendelea

[hariri | hariri chanzo]

Mimba ya fumbatio iliyoendelea inamaanisha hali ambapo mimba hiyo imeendelea zaidi ya wiki 20 za ujauzito.[11] Katika hali hizo, uzazi hai umeripotiwa, hivyo katika taarifa kutoka Nigeria kumekuwa na uzaaji wa watoto wanne hai kati ya mimba 20 za fumbatio 20.[2]i Mara nyingi, hata hivyo, mimba ikiendelea kukua usaidizi kwa kijusi huhatarishwa na kijusi hufa. Mgonjwa anaweza kubeba kijusi kilichokufa lakini hawezi kuhisi uchungu wa kuzaa. Baada ya muda, kijusi hupitia ukalisishaji na kuwa lithopedioni.

Kwa ujumla inapendekeza kufanya laparotomia mimba ya fumbatio inapotambuliwa.[4] Hata hivyo, kama mimba imezidi wiki 24 na mtoto yu hai na mifumo ya usaidizi wa kimatibabu ipo, uangalizi makini inaweza kufanyika kumfikisha mtoto anapoweza kujitegemea (wiki 34-36 ).[4] Wanawake wenye mimba ya fumbatio hawawezi kuhisi uchungu wa kuzaa Uzalishaji katika hali ya mimba ya fumbatio iliyoendelea hufanywa kwa laparotomia. Uwezekano wa kuishi kwa mtoto huwa umepunguzwa na viwango vya vifo baada ya kuzaliwa huongezeka, ongezeko kati ya 40-95% vimeripotiwa.[12]

Watoto wa mimba za fumbatio mara nyingi huwa namatatizo ya kuzaliwa kutokana na mbano kufuatia kukosekana kwa kinga ya majimaji ya amnioni. Kiwango cha ulemavu na kuharibika umbo unakadiriwa kuwa 21%; uharibifu wa umbo wa kawaida ni kama vile usona fuvu isiyo umbopacha pamoja ulemavu wa viungo, ulemavu mwingi hulenga miguu na mikono na matatizo ya neva uti wa mgongo.[13]

Mara mtoto anapozaliwa udhibiti kondo huanza kutoa usaha au damu. Katika kujifungua kwa kawaida kujikaza kwa uterasi hutoa nguvu maalum inayodhibiti kupoteza damu hata hivyo, katika mimba ya fumbatio kondo iko juu ya tishu ambayo haiwezi kujikaza na jaribio la kuliondoa linaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi. Kijumla, isipokuwa kondo inaweza kufungwa au kuondolewa kwa urahisi amefungwa, inaweza kuwa bora kuliacha lilipo kuliko kuliondoa hivyo kuruhusu mageuzi ya kawaida.[3][4] Hatua hii inaweza kuchukua muda wa miezi minne na inaweza kufuatiliwa kwa kuangalia viwango vyaproteni ya korioni na viwango vya useleleaji. Matumizi ya methotrexate kuongeza kasi ya kumalizika kwa kondo una utata mkubwa kwa kuwa kiwango kikubwa cha kufa kwa tishu kunaweza kuunda sehemu ya kuambukizwa.[3] Mishipa ya kondo pia imezibwana na angiografia na ugandanji damu mishipani.[14]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Atrash HK, Friede A, Hogue CJR. "Abdominal Pregnancy in the United States: Frequency and Mortality". Obstet Gynecol (Machi 1887): 333–7. PMID 3822281. {{cite journal}}: Unknown parameter |Number= ignored (|number= suggested) (help); Unknown parameter |Volume= ignored (|volume= suggested) (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 Sunday-Adeoye I, Twomey D, Egwuatu EV, Okonta PI. "A 30-year review of advanced abdominal pregnancy at the Mater Misericordiae Hospital, Afikpo, southeastern Nigeria (1976-2006)". Arch Gynecol Obstet. 2009 Oct 30. PMID 19876640.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 KY Kun, PY Wong, MW Ho, CM Tai, TK Ng. "Abdominal pregnancy presenting as a missed abortion at 16 weeks' gestation" (PDF). Hong Kong Medical Journal 2000;6:425-7. PMID 11177167. Iliwekwa mnamo 25 Januari 2009.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 Maurice King, Peter C. Bewes, James Cairns, Jim Thornton (editors). "Primary Surgery; Volume One: Non-trauma. Chapter 8, Abdominal pregnancy". Bonn University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-21. Iliwekwa mnamo 2010-01-25. {{cite web}}: |author= has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  5. 5.0 5.1 Anderson PM, Opfer EK, Busch JM, Magann EF. "An Early Abdominal Wall Ectopic Pregnancy Successfully Treated with Ultrasound Guided Intralesional Methotrexate: A Case Report". Obstetrics and Gynecology International, Volume 2009 (2009), Article ID 247452, 3 pages. doi:10.1155/2009/247452Case Report. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-11-01. Iliwekwa mnamo 2010-10-18. {{cite journal}}: Check |doi= value (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  6. Chui AK, Lo KW, Choi PC, Sung MC, Lau JW. "Primary hepatic pregnancy". ANZ J Surg. 2001 Apr;71(4):260-1. PMID 11355741.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  7. Yagil Y, Beck-Razi N, Amit A, Kerner H, Gaitini D. "Splenic Pregnancy: The Role of Abdominal Imaging". J. Ultrasound Med., Vol. 26, Issue 11, 1629-1632, 1 Novemba 2007. PMID 17957059.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  8. Norenberg DD, Gundersen JH, Janis JF, Gundersen AL. "Early pregnancy on the diaphragm with endometriosis". Obstet Gynecol. 1977 Mei;49(5):620-2. PMID 850582.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  9. 9.0 9.1 Krishna Dahiya, Damyanti Sharma. "Advanced Abdominal Pregnancy: A Diagnostic and Management Dilemma". Journal of Gynecologic Surgery. Juni 2007, 23(2): 69-72. doi:10.1089/gyn.2007.B-02259-1.
  10. Tromans PM, Coulson R, Lobb MO, Abdulla U. "Abdominal pregnancy associated with extremely elevated serum alphafetoprotein: case report". Br J Obstet Gynaecol 1984; 91:296. PMID 6200135.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  11. White RG (Machi 1989). "Advance Abdominal Pregnancy – A Review of 23 Cases". Irish Journal of Medical Science. 158 (3): 77–8. PMID 2753657. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-14. Iliwekwa mnamo 2010-10-18. {{cite journal}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  12. Martin JN Jr, Sessums JK, Martin RW, Pryor JA, Morrison JC. "Abdominal pregnancy: current concepts of management". Obstet Gynecol. 1988 Apr;71(4):549-57. PMID 3281075.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  13. Stevens CA. "Malformations and deformations in abdominal pregnancy". American journal of medical genetics 1993, vol. 47, no8, pp. 1189-1195. PMID 8291554.
  14. Cardosi RJ, Nackley AC, Londono J, Hoffman MS. "Embolization for advanced abdominal pregnancy with a retained placenta. A case report". Reprod Med. 2002 Oct;47(10):861-3. PMID 12418072.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]