Matsuo Bashō

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Basho mjini Ogaki

Matsuo Munefusa anayejulikana pia kama Matsuo Bashō (1644 - 28 Novemba 1694) alikuwa mshairi nchini Japani.

Husifiwa kama mshairi mashuhuri wa kipindi cha nasaba ya Edo. Amesifiwa hasa kwa ajili ya mashairi yake aina ya haiku ambayo ni mashairi mafupi yenye silabi 5-7-5. Haiku zake zinaandikwa mara nyingi kwenye majengo au sanamu nchini Japani.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Iga kwenye kisiwa kikuu cha Honshu upande wa magharibi wa Tokyo mnamo 1644 katika familia ya makabaila wadogo wa samurai. Alijifunza mwenyewe kazi ya vita kama samurai akaiacha badaye kuwa mwandishi na mashiri akadumisha maisha yake kama mwalimu. Alizunguka kote nchini Japani. Alijenga nyumba yake mjini Fukagawa kando la mjini wa kifalme wa Edo (leo: eneo la Tokyo) alipopanda mgomba bustani mwake akaipenda na kujiita "Basho" kwa sababu mgom ba kwa Kijapani ni "basho".

Aliaga dunia katika nyumba wa mwanafunzi wake akiwa safarini. Kabla ya kufa alitunga haiko ya mwisho:

Tabini yande / yume ha kareno wo / kake meguru
Safarini nimegonjeka
Ndoto yangu ni kuzunguka
shamba linalojaa manyasi makavu
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matsuo Bashō kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.