Mason Ferlic
Mandhari
Mason Ferlic (amezaliwa Agosti 5, 1993)[1] ni mkimbiaji wa masafa marefu kutoka nchini Marekani.
Mnamo mwaka 2019 alishiriki katika mbio za wanaume waandamizi kwenye Mashindano ya Dunia ya IAAF ya mwaka 2019 yaliyofanyika Aarhus, Denmark[2] nakumaliza katika nafasi ya 76.Mnamo 2021, alishika nafasi ya tatu katika mbio za mita 3000 za kuruka viunzi kwenye majaribio ya Olimpiki ya Merika.[3] Alishindana katika mashindano ya wanaume ya mbio za mita 3000 za kuruka viunzi kwenye Olimpiki za msimu wa joto za 2020 zilizofanyika huko mjini Tokyo, Japani.
Ferlic ni kocha msaidizi wa kujitolea katika Chuo chake cha Alma Mater, Chuo Kikuu cha Michigan.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mason FERLIC | Profile | World Athletics". worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-10-05.
- ↑ https://media.aws.iaaf.org/competitiondocuments/pdf/6265/AT-XSE-M-f----.RS6.pdf?v=-1530503012
- ↑ Joel Odom | The Oregonian/OregonLive (2021-06-25). "Hillary Bor wins steeplechase, Mason Finley tops discus field at U.S. Olympic track and field trials: Day 8 live updates recap, results". oregonlive (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-10-05.