Nenda kwa yaliyomo

Maski la mazoezi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maski la mazoezi (kwa Kiingereza: training mask) ni vazi linalovaliwa katika uso na wakimbiaji wanapofanya mazoezi yao. Vazi hilo huwakinga na baridi jingi. Vilevile huwasaidia kujiandaa vizuri kwa kupumua hewa kidogo.

Umuhimu wa maski la mazoezi kwa kupumua

[hariri | hariri chanzo]

Wakimbiaji wanapokimbia inawafaa kupata hewa kidogo sana. Iwapo watafanya mazoezi pahala ambapo kuna hewa jingi, huenda wakashindwa kukimbia pahala kusipo na hewa nyingi. Kwa wakati mwingi mashindano ya mbio hufanywa kunako milima na kwa sababu hii, hewa ya oksijeni huwa ni nadra sana. Mkimbiaji basi inafaa ajiandae vizuri asije kuhema sana ama hata kushindwa kukimbia kwa mashindano hayo.

Wakimbiaji wasio na maski la mazoezi huenda wakaanguka na hata kuzimia wakati wa mashindano maana miili yao inakosa okisijeni (athlete collapse).

Yaliyo muhimu kwa maski la mazoezi

[hariri | hariri chanzo]

Maski la mazoezi huundwa kwa njia mwafaka sana ili mkimbiaji aweze kuitumia bila shida kubwa. Maski hili huwa na sifa kama hizi:

1.      Nyepesi sana.

2.      Rahisi kusafisha na isinate vumbi

3.      Ishike kichwa vizuri

4.      Nyororo isikwaruze uso.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Maski la mazoezi kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.