Masasi (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Masasi mjini)

Masasi ni mji katika Mkoa wa Mtwara kwenye kusini mashariki ya Tanzania. Tangu mwaka 2012 ina halmashauri yake[1] na kuwa na hadhi ya wilaya.

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, eneo la mji lilikuwa na wakazi wapatao 102,696 waishio humo. [2] . Wakati wa senda mji ulikuwa na kata 12[3].

Eneo la mji ni takriban 400 km². Wakazi wengi hujishughulika na kilimo pamoja na biashara ya mazao ya kilimo.

Mazao makuu ya biashara ni pamoja na ufuta, karanga, choroko, korosho na njugumawe. Kwa upande wa mazao ya chakula ni mahindi, mtama, mpunga pamoja na muhogo.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Town Council
  2. Sensa ya 2012, Mtwara Region - Masasi Town Council
  3. Tovuti ya Halmashauri ya Mji inataja idadi ya kata 14 ilipotazamiwa Septemba 2015

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Masasi Mjini - Mkoa wa Mtwara - Tanzania

Chanikanguo | Jida | Marika | Matawale | Migongo | Mkomaindo | Mkuti | Mtandi | Mumbaka | Mwenge Mtapika | Napupa | Nyasa | Sululu | Temeke

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Masasi (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.