Nenda kwa yaliyomo

Margaret Thatcher

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Margaret Thatcher

Margaret Hilda Thatcher (alizaliwa Margaret Hilda Roberts 13 Oktoba 19258 Aprili 2013) alikuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia 1979 hadi 1990 na mwanamke wa kwanza aliyeshika cheo hiki.

Alichaguliwa kama mgombea na kiongozi wa chama cha Conservative Party. Aliendesha mabadiliko mengi ya kiuchumi na kisiasa. Baada ya Argentina kuvamia visiwa vya Falkland (Malvina) alituma manowari na wanajeshi waliorudisha visiwa chini ya utawala wa Uingereza.

Kutokana na siasa hizi alipewa jina la "Iron Lady" (mwanamke wa shoka).

1989-1990 alijaribu kuanzisha aina mpya ya kodi na jaribio hili lilisababisha ghasia nchini. Kwa hiyo aliona upinzani mkubwa ndani ya chama chake na tar. 22 Novemba 1990 alitangaza ya kwamba alijiuzulu akafuatwa na John Major.

Tangu 1951 aliolewa na Sir Dennis Thatcher akazaa watoto wawili mapacha.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Margaret Thatcher kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.