Manza Bay

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Manza Bay Ni ghuba iliopo nchini Tanzania. Inapatikana ufukweni mwa bahari ya Hindi, maili 10 (kilomita 16) kaskazini mwa mji wa Tanga.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kwenye kampeni ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia katika Afrika Mashariki, Jeshi la Wanamaji la Kifalme lililinda meli HMS Hyacinth isishambuliwe na kuharibiwa na meli ya Wajerumani kutoka ghuba ya Manza ilikua tarehe 14 mwezi wa nne 1915. ilikuwa meli namba 3,587 GRT ya Uingereza ya shehena, Rubens, na mamlaka ya Ujerumani ambayo walikamata meli hiyo huko Hamburg mwaka 1914. Jeshi la Wanamaji la Ujerumani lilimficha Rubens kama meli ya mizigo ya Denmark Kronborg na kumtuma kujaza cruiser SMS Königsberg katika Bahari ya Hindi.[1]

Kikundi cha Wajerumani walifanikiwa kuifunga meli yao kwenye ghuba, wakaokoa silaha zao na risasi kutoka kwa shehena ya Rubens, na kuiacha.Silaha na risasi zilisaidia vikosi vya nchi kavu vya Ujerumani katika Afrika Mashariki kuendelea na kampeni yao kupinga dhidi ya vikosi vya Uingereza na Dola.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 https://wrecksite.eu/wreck.aspx?102286