Nenda kwa yaliyomo

Malaika Mihambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malaika Mihambo mwaka 2011.
Malaika Mihambo mwaka 2013.

Malaika Mihambo (alizaliwa Heidelberg, Ujerumani, 3 Februari 1994) ni mwanariadha kutoka nchini Ujerumani aliyeshinda mashindano ya kilimwengu ya kuruka chini mwaka 2019.

Kwenye Michezo ya Olimpiki 2021 huko Tokyo alipata medali ya dhahabu kwenye mashindano ya kuruka chini.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Baba yake Malaika ni mtu wa Zanzibar na mama yake ni Mjerumani. Tangu umri wa miaka 8 aliingia katika michezo ya riadha. Alifuata masomo ya shule kwake Heidelberg hadi kumaliza A-levels mwaka 2012 akajiunga na Chuo Kikuu cha Mannheim aliposoma elimu ya siasa[1]. Mwaka 2019 alianza kusoma elimu ya mazingira. Anajitolea katika shule yake ya zamani kwenye mradi wa kusaidia watoto kuendelea uwezo wao wa riadha. Malaika anapenda muziki akipiga kinanda[2].

Alipokuwa na miaka 14 alianza kushiriki katika mashindano kwenye ngazi ya kitaifa Ujerumani akionyesha uwezo wake katika fani za mbio na kuruka chini. Kwenye mashindano ya kimataifa ya riadha kwa vijana mwaka 2011 alichukua nafasi ya 9 akaendelea kushiriki paia katika miaka iliyofuata. Mwaka 2013 alishinda medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha ya Ulaya kwa vijana.

Kwenye mashindano ya riada ya kilimwengu 2013 mjini Moscow aliruka mita 6.94 akipata nafasi ya 18. Mwaka 2014 aliboresha matokeo yake hadi kufikia mita 6.90.

Mwaka 2016 alishiriki katika Michezo ya Olimpiki pale Rio de Janeiro alipofikia mita 6.95 na kushika nafsi ya nne katika finali ya kuruka chini.

Mwaka 2018 alipata nafasi ya tano katika mashindano ya riadha ya ukumbini na kupata medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha ya Ulaya.

Kwenye mashindano ya riadha ya kilimwengu mjini Doha kwenye Oktoba 2019 aliboresha umbali wake katika kuruka chini kufikia mita 7.30 akashinda nafasi ya kwanza.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Mihambo Malaika, tovuti ya Chuo Kikuu cha Mannheim, Misaada ya masomo mwaka 2012-13
  2. Malaika Mihambo: Meisterin im Sand mit Interessen weit über den Sport hinaus Archived 23 Juni 2023 at the Wayback Machine. (Malaika Mihambo, mbingwa katika mchanga akiwa na moyo wa kupenda mambo mengi), tovuti ya Leichtathletik.de, habari ya 4 Oktoba 2019

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malaika Mihambo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.