Nenda kwa yaliyomo

Makumbusho ya Bonde la Oltupai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jumba la makumbusho ya Bonde la Oltupai.

Makumbusho ya Bonde la Oltupai (kwa Kiingereza: Olduvai Gorge Museum) yanapatikana katika hifadhi ya Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania katika bonde la Oltupai.

Makumbusho haya yaliweza kuvumbiwa na Mary Leakey na kwa sasa yapo chini ya mamlaka ya kitengo cha mambo ya kale ya utamaduni ya Tanzania na inasimamiwa na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro. Ni jumba la makumbusho lililowekwa kwa ajili ya kuthamini na kuelewa maeneo ya Olduvai Gorge na Laetoli.