Majek Fashek

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Majekodumni Fasheke ambaye jina lake maarufu ni Majek Fashek ni mwanamuziki wa Reggae toka Nigeria.

Majek Fashek alianza kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipotokea kwenye kipindi cha televisheni nchini Nigeria. Baada ya hapo alifanya ziara za kimuziki na kundi lililoitwa The Mandators. Mwaka 1987 alijitoa kwenye kundi hilo na kuwa peke yake. Alipata jina kubwa nchini Nigeria hasa kufuatia wimbo wake ulioitwa 'Send Down the Rain.' Alifanikiwa kupata tuzo sita za PMAN na baada ya hapo kusaini mkataba na kampuni ya CBS ya Nigeria. Baadaye alijitoa toka kwenye kampuni hiyo na kujiunga na Island Records, kampuni ambayo ina jina kubwa katika muziki wa Reggae duniani. Alipojiunga na kampuni hiyo alirekodi wimbo wa Bob Marley wa Redemption Song.


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Musical notes.svg Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani wa Afrika bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Majek Fashek kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.