Majadiliano ya mtumiaji:Jerryn159
Asante, Jerry, kwa kazi yako. Nimeboresha makala ya Tarakilishi upande wa taratibu na lugha za Wikipedia. Sasa endelea wewe na utaalamu wako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:48, 30 Januari 2016 (UTC)
Majina ya wanyama
[hariri chanzo]Jerry salaam. Asante sana kwa kuchangia makala kuhusu wanyama wa baharini. Lakini tafadhali hakikisha majina unayotumia. Unaweza kupendekeza majina mapya endapo hakuna majina kwa Kiswahili, lakini majina yaliyoko yana kipaumbele. Kwa mfano "papa kichwanyundo": ulibuni jina hili au linatumika kweli? Mimi, silijua. Ninajua "papa mbingusi" na "papa nyundo". ChriKo (majadiliano) 16:46, 3 Novemba 2016 (UTC)
- Asante ndugu. Nitazingatia ushauri wako. tafadhali naomba viungo vya wavuti za kamusi ili niwe nahakiki majina. siku njema
- Ok, karibu sana. Kupata majina rasmi si rahisi. Kunahitaji kazi nyingi kwa sababu hakuna kamusi moja iliyo na majina yote. Lakini unaweza kuanza na Identification guide na Fishbase. ChriKo (majadiliano) 15:16, 5 Novemba 2016 (UTC)
Namna ya kutafsiri
[hariri chanzo]Bwana Jerryn, salamu na asante kwa michango yako! Nimeangalia makala yako kuhusu Isopodi Mkubwa na kufanya masahihisho kadhaa katika sehemu ya kwanza. Naomba unisamehe nikijaribu kukupa ushauri ingawa hujaniuliza!
Nimeona ya kwamba umejaribu kutafsiri kimakini en:Giant isopod. Hii ilileta matatizo kadhaa. Ushauri wangu ni huu: chukua makala ya Kiingereza kama mfano lakini usijaribu kutafsiri neno-kwa-neno.
Maana njia hii inaleta matatizo yafuatayo: muundo wa sentensi ni tofauti katika kila lugha, kwa hiyo unaweza kupata sentensi ambayo haieleweki kabisa.
Kwa Kiingereza wanatumia mara nyingi nomino pale ambako Kiswahili kinapendelea vitenzi.
Hasa katika matini kuhusu habari za sayansi utaona unapaswa kutafuta msamiati na labda unaacha kwanza maneno ya Kiingereza katika sentensi inayotafsiriwa na baadaye unasahau kuyasafisha tena - hii ilitokea mara kadhaa katika sehemu niliyochungulia.
Kwa hiyo soma makala ya Kiingereza, angalia kama kuna makala ileile pia katika simple.wikipedia.org au kwa lugha nyingine unayojua, tafakari jinsi gani hao wengine wanaeleza jambo, halafu andika habari kwa maneno yako. (binafsi nikitunga makala kuhusu fizikia au kemia, najaribu kutafuta pia "for dummies", hivyo "transistor for dummies, resistance for dummies" maana kama iko mara nyingi wana njia nzuri zaidi ya maelezo kuliko makala za en:wikipedia wanapojaribu kuiga Kiingereza cha kitaalamu - ambacho hakisaidii utafsiri)
Ukikuta sentensi ngumu mno - usitafsiri! Uikatekate kwa sentensi mbili au tatu au fupisha kama si lazima sana. Vivyo hivyo ukikuta maneno mengi ambayo hujui namna ya kutafsiri - fupisha tu kama si lazima kabisa, au eleza kitu kwa maneno yako. (Hapo nimefuta sentensi kuhusu "woodlouse" kwa sababu sijui jina lake kwa Kiswahili nikaona si lazima sana), Kwa jumla afadhali zuwe na makala fupi inayosomeka kuliko makala ndefu ambayo haieleweki na kufukuza wasomaji wetu. Kipala (majadiliano) 12:29, 6 Novemba 2016 (UTC)
Share your experience and feedback as a Wikimedian in this global survey
[hariri chanzo]Hello! The Wikimedia Foundation is asking for your feedback in a survey. We want to know how well we are supporting your work on and off wiki, and how we can change or improve things in the future.[survey 1] The opinions you share will directly affect the current and future work of the Wikimedia Foundation. You have been randomly selected to take this survey as we would like to hear from your Wikimedia community. To say thank you for your time, we are giving away 20 Wikimedia T-shirts to randomly selected people who take the survey.[survey 2] The survey is available in various languages and will take between 20 and 40 minutes.
You can find more information about this project. This survey is hosted by a third-party service and governed by this privacy statement. Please visit our frequently asked questions page to find more information about this survey. If you need additional help, or if you wish to opt-out of future communications about this survey, send an email to surveys@wikimedia.org.
Thank you! --EGalvez (WMF) (talk) 20:51, 13 Januari 2017 (UTC)
- ↑ This survey is primarily meant to get feedback on the Wikimedia Foundation's current work, not long-term strategy.
- ↑ Legal stuff: No purchase necessary. Must be the age of majority to participate. Sponsored by the Wikimedia Foundation located at 149 New Montgomery, San Francisco, CA, USA, 94105. Ends January 31, 2017. Void where prohibited. Click here for contest rules.
Kurasa mpya
[hariri chanzo]Jerry salaam. Sikuona kurasa mpya kutokana na mkono wako tangu muda mrefu. Ni nini kinachoendelea? Natumaini hukutuacha. Ningefurahi kushirikiana na wewe juu ya makala kuhusu wanyama wa baharini. ChriKo (majadiliano) 14:52, 5 Februari 2017 (UTC)
Your feedback matters: Final reminder to take the global Wikimedia survey
[hariri chanzo](‘’Sorry to write in English’’)
Hello! This is a final reminder that the Wikimedia Foundation survey will close on 28 February, 2017 (23:59 UTC). The survey is available in various languages and will take between 20 and 40 minutes. Take the survey now.
If you already took the survey - thank you! We won't bother you again.
About this survey: You can find more information about this project here or you can read the frequently asked questions. This survey is hosted by a third-party service and governed by this privacy statement. If you need additional help, or if you wish to opt-out of future communications about this survey, send an email through EmailUser function to User:EGalvez (WMF). About the Wikimedia Foundation: The Wikimedia Foundation supports you by working on the software and technology to keep the sites fast, secure, and accessible, as well as supports Wikimedia programs and initiatives to expand access and support free knowledge globally. Thank you! --EGalvez (WMF) (talk) 07:30, 23 Februari 2017 (UTC)