Majadiliano:Wangari Maathai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Tarehe 27 Aprili, 2007, 128.12.68.114 aliandika makala ifuatavyo, lakini angalia mashaka kuhusu makala hiyo kwenye majadiliano ya makala kwa ufutaji:

Mwaka ulikuwa 1989, na serikali ya Kenya ilitaka kujenga jengo kubwa la ghorofa thelathini katika bustani ya Uhuru park, huko mjini Nairobi. Wangari Maathai, pamoja na shirika lake, liitwalo Greenbelt Movement (GBM), walisimamisha huu mradi, na wananchi wote ambao hutumia bustani hii, walisherekea. Maathai alikuwa mtu mashuhuri wa kutajika na watu walimsifu. Katika utawala wa rais Daniel Arap Torotich Moi, Maathai alifungwa gerezani mara nyingi ambako polisi walimchapa. Hii ilikuwa kwa sababu ya kazi yake ya kujaribu kusimamisha serikali ambayo hujaribu kushika ardhi ya umma, na bidii zake kurudisha haki na uaminifu nchini Kenya. Maathai ni mwanamke aliye na nguvu zaidi, kwa hivyo hata baada ya kufungwa gerezani, aliendelea kubabaka na hatimaye amefaulu. Kufaulu kwake kulikuja katika mwaka wa 2002 ambapo or wakati wananchi wa Kenya walipiga kura, na walichagua rais Mwai Kibaki. Baada ya miaka ishirini na tano, Moi aliondolewa na demokrasi ya kweli ilikuja Kenya. Kibaki alichagua Maathai awe waziri msaidizi akishugulikia mazingira. Hatimaye serikali ya Kenya ilithamini sifa za Wangari Maathai. Wangari alionyesha wananchi wa Kenya kwamba ukibabaka na ukigoma, utafaulu, kwa sababu “penye nia pana njia .”

Elimu na Tuzo

Maathai amekuwa mtu maarufu katika miaka mingi huko Kenya, lakini kutoka mwaka wa 2004 amekuwa maarufu kote duniani. Hii ni kwa sababu katika mwaka huo, Maathai alichaguliwa kutuzwa na Zawadi ya Nobel ya Amani. Alichaguliwa kwa sababu ya kazi yote aliyofanya pamoja na shirika lake ambalo alianza katika mwaka wa 1977. Tangu mwaka huo, shirika lake limepanda miti milioni thelathini kusaidia wananchi mashambani kufukuza ukame. Pia, GBM imesaidia na imefundisha wanawake kutoka jamii nyingi kuhusu haki zao, gonjwa la ukimwi, mambo ya mazingira na kuhusu maendeleo endelevu. Kweli shirika lake, limefanya kazi njema nchini Kenya. Lakini Maathai ni mwanamke ambaye kwaye shirika hii ilianzwa. Yote kutoka kwa mwanamke ambaye awali alikuwa mnyenyekevu zaidi. Wangari Muta Maathai ni Mkikuyu ambaye alizaliwa mwaka wa 1940 katika chengo cha Ihithe, sehemu ya Nyeri. Sehemu ya Nyeri inayo watu elfu mia sita sitini na moja, imo mkoa wa kati nchini Kenya. Maathai alidurusu shule ya msingi ya Ihithe sehemu ya Nyeri. Halafu alisafiri Limuru ambako alijiunga na shule ya sekondari ambayo inaitwa Loreto Convent, Limuru. Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari, alienda ng’ambo kusoma biolojia nchini Ujerumani na pia nchini Marekani. Alipata shahada ya kwanza ya biolojia kutoka chuo kikuu cha Benedictine katika mwaka wa 1967. Kufuatia hii aliendelea na masomo yake kwa chuo kikuu cha Pittsburg, ambako alipata shahada ya pili. Halafu akarudi Nairobi na akapata PHD yake kutoka chuo kikuu cha Nairobi kwa msomo ya udaktari wa wanyama. Baada ya hiyo, katika mwaka 1977, Maathai alikaa huko chuo kikuu cha Nairobi kufanya kazi ya profesa msaidizi wa anatomia ya wanyama. Alikuwa mwanamke wa kwanza kupata kazi ya profesa katika chuo kikuu cha Nairobi. Kweli ilikuwa mapato makubwa. Juu ya hayo, baina ya miaka ya 1976 na 1987 alikuwa mwanachama wa Maendeleo Ya Wanawake, na alichaguliwa mwenyekiti wa baraza (baraza la nini ama baraza gain?) sawa katika mwaka wa 1981. Pia baina ya miaka ya 1983 na 2006, Maathai ametuzwa zaidi ya tuzo kubwa thelathini. Nimesema tayari alituzwa na Zawadi ya Nobel ya Amani (2004) lakini pia tuzo zake zinajumuisha Tuzo ya Mwanamke ya Dunia (1983), Tuzo ya Mazingira ya Goldman (1991), “Elder of the Burnning spear” (2003) kutoka serikali ya Kenya, na Legion D’Honneur (2006) kutoka serikali ya Ufaransa. Si rahisi kupata tuzo nyingi kama hizi; kweli yeye ni shujaa.

Shirika lake la GBM

Ilikuwa katika kazi yake na Maendeleo Ya Wanawake ambapo Maathai aliamua kuanza shirika lake la GBM. Alisema, “Shabaha ya GBM ni kujenga jamii ya watu ambao wangetaka kufanya kazi kwa akili, kuendelea kuboresha posho zao, na pia kutengeneza nchi ya Kenya iwe safi, pamoja na mazingira ya rangi ya kijani. Kwa siku za usoni, GBM, ingetaka kufanya kazi ya kupitisha maarifa ya GBM kwa nchi nyingine za dunia .” Kwa hivyo Maathai alianza kufanya kazi na wanawake wa mashambani, na aliwafundisha njia nzuri za kupanda miti. Hata leo, wanawake hao wanaendelea kueneza ujumbe wa Maathai na GBM. Pia kupitisha maarifa ya shirika hili nchini Kenya, GBM imeanzisha shirika jingine ambalo linaitwa Greenbelt Movement International (GBMI). Tovuti ya GBMI inasema, “Nia ya GBMI ni dunia ambamo mazingira, nafasi ya demokrasi, na amani ni thabiti na wananchi wote wa dunia wana uwezo wa kufaulu .” Maathai ni balozi mkubwa wa Kenya na angependa kukinga mazingira na kusaidia watu maskini kote duniani.

Ndoa na familia

Katika mwaka wa 1969 Wangari Muta (jina lake la kimwanamwali) alifunga harusi na Mwangi Mathai, mwanasiasa wa Kenya. Walakini, baada ya miaka michache Wangari aliachwa na mume wake. Hii ilikuwa kwa sababu Mwangi aligundua kwamba Wangari Maathai si mwanamke Mwafrika Mashariki wa kawaida, hasa katika miongo ya 1960 na 1970. Katika nyakati hizo hasa wanawake walioishi mashambani, lakini pia wengine walikuwa mjini, walitarajiwa kuwa bibi. Walitakiwa kukaa nyumbani ili waweze kulea watoto na kuchunga nyumba. Lakini au walakini, Maathai aliamua kujielimisha na kufuata ndoto yake kusoma ng’ambo, kupata shahada na kurudi Kenya kuania haki za wanawake wa Afrika Mashariki. Kwa hivyo yeye ni mtu mwerevu anayeongea moja kwa moja. Mwangi Mathai ametajwa kusema kwamba Wangari “ameelimishwa zaidi, ana nguvu zaidi, amefanikiwa zaidi, ni mtu mgumu zaidi na yeye (Mwangi) hawezi kuamuliwa” . Ile taarifa ya Mwangi Mathai ilionyesha kwamba Mwangi ni mtu dufu na hawezi kukubali mke wake awe na akili nyingi. Wakati Wangari alikuwa ameolewa, alizaa watoto watatu. Kinfunguamimba anayeitwa Waweru alizaliwa katika mwaka wa 1974. Alifuatwa na mtoto ambaye aliitwa Wanjira na Wanjira alifuatwa na kitindamimba anayeitwa Muta. Leo, Wanjira Maathai anafanya kazi pamoja na mamake; yeye ni jamaa ya kimataifa ya GBM. Binafsi ninafurahi wakati ninasikia mama na binti wanafanya kazi pamoja, ambako wanasaidia watu na wanajaribu kujenga dunia safi.