Majadiliano:Tumbaku

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Salaam tena mzee wangu. Hizi wanaita "TUMBAKU". Tangu utotoni mwangu hadi leo sijasikia jina la Tumbako. Labda ile Kidhungu zaidi! Wazo tu, mzee wangu.--MwanaharakatiLonga 14:30, 3 Juni 2014 (UTC) [jibu]

Haya, mwalimu wangu! Wajua Wamasai huchanganya z na s, wengine l na r, mimi o na u. Kipala (majadiliano) 16:37, 3 Juni 2014 (UTC)[jibu]
Naam, kwa Kiswahili (kama kwa lugha nyingine) o na u huchanganywa. Ni kweli, Watanzania wengi husema "tumbaku" lakini watu wengine husema "tumbako" na neno hili limo katika kamusi nyingi. ChriKo (majadiliano) 21:08, 3 Juni 2014 (UTC)[jibu]
Asante kwa kuchangia! Sasa ibaki vile nilivyobadilisha? Maana nimechukua tumbako kutoka "mtumbako" lakini hata makala ile niliwahi kuanzisha. Nikiangalia KKK/ESD online http://kess.co.tz/eng-swa/m.html ni tumbaku pia nikifanya google,check: tumbaku 213,000, tumbako 7,280 results. Ibaki, je? Kipala (majadiliano) 21:15, 3 Juni 2014 (UTC)[jibu]
Sawasawa tu, ibaki. ChriKo (majadiliano) 21:23, 3 Juni 2014 (UTC)[jibu]
Ahsanteni kwa kunisikiliza!--MwanaharakatiLonga 12:25, 4 Juni 2014 (UTC)[jibu]