Majadiliano:Teresa wa Yesu

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jina la makala[hariri chanzo]

Nisipokosei Teresa hujulikana zaidi kwa jina "Teresa wa Avila" kimataifa (mimi mwenyewe awali sikumtabua kwa jina hili). Isingekuwa afadhali kuhamisha makala kwa jina hili? --Kipala (majadiliano) 07:37, 1 Novemba 2009 (UTC)[jibu]

Nakubali kwamba wengi wanamfahamu kama Teresa wa Avila, lakini mwenyewe hakujiita hivyo, na Kanisa lake limeamua kutumia jina alilolitumia mwenyewe kama Mkarmeli. Ukiangalia wiki za lugha nyingine, baadhi zinatumia hili, baadhi hili. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:03, 8 Novemba 2009 (UTC)[jibu]
Kuhusu nukuu niliyoiweka mwanzoni, niliiga wiki ya Kiitalia, ambapo kurasa nyingi, na si za watakatifu tu, zinaweza zikaanza na dondoo. Kama katika wiki ya Kiswahili haipendezi, sawa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:18, 8 Novemba 2009 (UTC)[jibu]